Na Janeth Raphael MichuziTv
Bodi ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza matokeo ya mitihani ya 33 ya taaluma ya Mnyororo wa Ugavi iliyofanyika nchini kuanzia Mei 11 hadi 15, 2026, huku jumla ya watahiniwa 682 sawa na asilimia 43.7 wakifaulu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfrey Mbanyi, amesema jumla ya watahiniwa 1,632 walikuwa wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo, lakini watahiniwa 1,559 ndio walioifanya, huku watahiniwa 73 wakishindwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.
Amesema kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo, watahiniwa 682 (asilimia 43.7) wamefaulu, watahiniwa 773 (asilimia 49.6) wamepata hadhi ya referral na watarudia baadhi ya masomo yao, huku watahiniwa 104 (asilimia 6.7) wakifeli na kulazimika kuanza upya masomo katika ngazi husika.
Mbanyi amesema bodi inawahimiza watahiniwa waliopata referral na wale waliofeli kujisajili kwa ajili ya mitihani ya kati (Mid-Session Examinations) itakayofanyika Agosti 24 hadi 28, 2026, au kushiriki mitihani ya Novemba 2026 ili kuboresha matokeo yao.
Ameongeza kuwa dirisha la usajili kwa ajili ya mitihani ya kati litafunguliwa kuanzia Julai 1 hadi Agosti 7, 2026.
Aidha, aliwataka watahiniwa wenye hadhi ya Last Chance Referral kutumia ipasavyo fursa ya mitihani ya kati au ya Novemba 2026, kwani ndiyo nafasi yao ya mwisho ya kukamilisha ngazi za mitihani wanazosomea.
Katika hatua nyingine, PSPTB imewaalika watahiniwa wote wa ngazi ya CPSP II waliofaulu kushiriki warsha ya utafiti itakayofanyika mwishoni mwa Julai 2026, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya hatua zinazofuata katika taaluma yao.
Mbanyi pia ametoa wito kwa wahitimu wa vyuo vikuu vya ndani na nje ya Tanzania kujisajili kufanya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB ili kupata sifa zinazotambulika kitaaluma katika fani ya Ununuzi na Ugavi.
Vilevile, amewataka wazazi, wadhamini na waajiri kuendelea kuwawezesha watahiniwa kwa kulipia ada za maandalizi na mitihani, akisema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi na maarifa katika sekta ya ununuzi na ugavi.
Hata hivyo, PSPTB imesisitiza kuwa haitavumilia vitendo vya ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani. Mbanyi alisema bodi itaendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya watakaobainika kufanya udanganyifu au kukiuka maadili ya mitihani.
Alieleza kuwa adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa kanuni ni pamoja na kufutwa kwa matokeo ya mitihani, kusimamishwa kushiriki mitihani kwa kipindi cha hadi miaka mitatu, pamoja na adhabu nyingine za kisheria ikiwemo faini au kifungo cha jela kulingana na uzito wa kosa.
Kwa mujibu wa PSPTB, hatua hizo zinalenga kulinda uadilifu wa mitihani na kuhakikisha taaluma ya Ununuzi na Ugavi inaendelea kujengwa katika misingi ya maadili, weledi na uwajibikaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...