RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 13 Juni 2026, amejumuika na wanafamilia, ndugu, jamaa, wasanii, na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya msanii mkongwe, marehemu Issa Joseph Mohamed, maarufu kwa jina la Mzee Onyango, yaliyofanyika Kawe , Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwemo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, pamoja na wasanii wa fani mbalimbali na wananchi waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

Mara baada ya kuwasili, Rais Dkt. Mwinyi alisaini kitabu cha maombolezo na kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia.

Marehemu Issa Joseph Mohamed alizaliwa tarehe 14 Aprili 1950 na kufariki dunia tarehe 11 Juni 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Jijini Dar es Salaam.

Wakati wa uhai wake, marehemu alipata umaarufu mkubwa kupitia kazi zake za filamu na maigizo na kujizolea heshima kubwa miongoni mwa Watanzania kwa jina la Mzee Onyango.

Marehemu amezikwa katika Makaburi ya Kondo, Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe. Amina.























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...