-Atoa maagizo lukuki ya kuboresha Mkoa huo kuelekea AFCON 2027.


-Ataka muonekano mzuri wa Jiji kwa kufanya usafi wa mazingira na kuondoa kabisa gereji bubu barabarani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa gereji na mafundi seremala kuondoa vyuma chakavu na samani chakavu maeneo ya barabarani ili jiji liwe nadhifu huku akiwataka Madiwani, wenyeviti wa mitaa,watendaji wa kata na mitaa pamoja na wakuu wa wilaya zote tano kushiriki kikamilifu katika ulinzi na usalama wa maeneo yao na Mkoa huo kwa ujumla ikiwemo kuanzisha vikundi vya sungusungu

Akizungumza katika katika kikao kazi maalum kilichokutanisha Madiwani, wenyeviti wa mitaa,watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wakuu wa wilaya zote tano za Mkoa huo Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila amesema vyuma hivyo chakavu kwenye maeneo ya barabara vimekuwa vikiharibu muonekano wa jiji huku pia akisisitiza serikali mkoani humo haitokuwa tayari kuona amani ya mkoa huo inavurugwa kwa kuwa mkoa huo ndio kitovu cha masuala ya kidiplomasia na uchumi

Aidha amezungumzia taarifa zinazosambaa mitandaoni juu ya uwepo wa watu wanaofikiria kufanya maandamano ambapo amewataka viongozi na mitaa na kata kuendelea kusimamia amani kwenye mitaa na kata zao

Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi wa wangazi za mitaa na kata kuimarisha usafi wa mazingira ili kuepukana na maradhi ya mlipuko na watambue kuwa Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON,hivyo haitokuwa vyema kuona heshima hiyo ambayo Taifa imepata inaharibiwa kutokana na uzembe kwenye suala la usafi na amewataka wakurugenzi kusimamia vyema sheria na kanuni za usafi wa mazingira ili kuimarisha usafi na kudhibiti tabia ya utupaji taka hovyo huku akisisitiza majengo ya barabarani kupaka rangi nyumba zao

Akizungumzia suala la mchakato wa uendeshaji wa dampo la pugu kinyamwezi kwa ubia na kampuni binafsi Chalamila ametoa muda wa hadi julai 30 kwa mchakato huo kuanza kwa mpango huo na amehimiza Halmashauri zote za jiji hilo kuwa na dampo la kutupia taka sanjari na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujua kutrndanisha taka na amepiga marufuku suala la ubandikaji wa picha za matangazo kwenue maeneo ya jiji hilo na amewstaka wakurugenzi kutotoa vibali vya bar kwenye makazi ya watu ikiwemo Masaki na Oystabay

Awali Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam Ndg Abdul Mhinte amesisitiza suala la anuani za makazi kutumika vyema kutambua watu na makazi yao ili kusaidia kuimarisha Amani.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...