Na Mwandishi Wetu

HALIMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe,Mkoani Pwani imeendelea kung'ara kwa kupata hati safi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serkali (CAG), kwa kipindi cha miaka minne mfurulizo.

Wilaya hiyo imepata hati safi katika mwaka wa fedha 2021/22 , mwaka wa fedha 22/23, mwaka wa fedha 23/24 na mwaka huu wa fedha wa 24/25.

Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la halmahauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe Abubakar Kunenge, amewapongeza viongozi wa wilaya na halimashauri hiyo kwa uwajabikaji.

Kunenge amesema hati safi hizo ziwe chachu kwa wilaya na halimashauri hiyo kutekeleza mikakati ya maendeleo na kupunguza changamoto za wananchi.

Ameeleza, hati safi ni lazima iakisi maendeleo yaliyopo katika halimashauri hivyo kuwataka viongozi na watendaji kuongeza nguvu katika kubuni vyanzo vya vipya vya mapato,ukusanyaji wa mapato na uwekezaji.

"Hati safi inatokana na ukaguzi wa hesabu za fedha zilivyo tumika kwa usahihi, hivyo Kisarawe ni lazima sasa mjielekeze katika kupanga bajeti ya kutekeleza mirdi ya maendeleo,"amesema Kunenge.

Amesema, Kisarawe inatakiwa kufanya jitihada kubwa za kuinuka kiuchumi kwani ina fursa nyingi zinazo vutia uwekezaji.

"Naomba tu ni wachane, Kisarawe kuna changamoto ya migogoro ya ardhi. Unaleta wawekezaji lakini wanakimbia kwa sababu ya migogoro.Malizeni migogoro yenu," amesema

Amebainisha Kisarawe inafursa za utalii na uchmbaji madini unaoweza kuvuta ujenzi wa viwanda hivyo kuongeza mapato.

"Mjiulize kwanini watu wanachimba madini hapa lakini hawajengi viwanda.Ondoeni migogoro.Madiwani msiogope kueleza wazi kuhusu wavamizi wa ardhi katika maneno yenu,"ameeleza Kunenge.

Mwenyekiti wa Baraza la Halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Aidan Kitare, alimhakishia mkuu huyo wa mkoa kuwa Halmashauri hiyo inamikakati kabambe ya kujikwamua kiuchumi, ikiwemo uwekezaji katika ardhi na usimamizi wa vyanzo vya mapato.

Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya CAG Mkoa wa Pwani, Faith Mutune, ameipongeza halmashaurihiyo kwa kupata hati safi na kuitaka kufunga hoja nane za ofisi hiyo zilizo salia.

Awali Mweka Hazina wa halmashauri hiyo ,Grace Maembe, alieleza utekelezaji wa hoja za CAG kwa mwaka 2024/25 kuwa zilikuwa 29, ambapo hoja 19 zimetekelezwa sawa na asilimia 66%, hoja nane zinaendelea kutekelezwa sawa na asilimia 28%, hakuna hoja isiyo tekelezwa, hoja mbili zimejirudia hivyo kufanya halmashauri hiyo kutekeleza kwa asiliomia 100 ya hoja zote za CAG.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...