Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Tanzania inaendelea kuwa salama, tulivu na yenye amani, huku akionya kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayehusika na vitendo vya kuvuruga utulivu wa nchi kupitia mitandao ya kijamii au kwa njia nyingine yoyote.
Akizungumza Bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Dodoma Mjini Paschal Chinyele aliyetaka kujua mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Maandamano yanayoratibiwa na watu wasiojulikana na kuleta taharuki nchini je kama serikali suala hilo wanalifahamu na itachukua hatua gani kulinda usalama wa watanzania?
Katambi amesema ni kweli kumekuwa na baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za upotoshaji, zenye uchochezi na zinazoweza kuzua taharuki kwa wananchi, jambo ambalo Serikali inalifuatilia kwa karibu.
Amesema Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepewa jukumu la msingi la kulinda amani na usalama wa nchi, hivyo hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha hali hiyo inadumishwa wakati wote.
"Tumeanza kufuatilia viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. Kila aliyepanga kuvuruga amani ya nchi kupitia mitandao ya kijamii au moja kwa moja katika jamii yetu atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria," alisema Katambi.
Aidha, Waziri huyo amesema Serikali imekuwa ikishuhudia baadhi ya mikusanyiko ya watu ikitumika kutoa kauli na taarifa zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi, hali ambayo haitavumiliwa.
Kutokana na hali hiyo, Katambi amemwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kutoa maelekezo kwa makamanda wote wa polisi kuanzia ngazi ya mikoa hadi kata kuimarisha mipango ya kiusalama katika maeneo yao.
Amesema ulinzi utaimarishwa kuanzia ngazi ya vitongoji hadi mitaa ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unaendelea kuimarika katika kipindi chote.
Katambi pia amekumbusha kuwa hivi karibuni Tanzania itakuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, yatakayohusisha wageni na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali, huku akisisitiza kuwa tukio hilo lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
"Katika kipindi hiki chenye matukio muhimu ya kitaifa na hizi chokochoko zinazoendelea, hatutaweza kumvumilia mtu yeyote atakayefanya vurugu za aina yoyote. Ninawahakikishia wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku kwa sababu vyombo vya usalama vimejipanga kikamilifu kudhibiti uhalifu na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama," amesema.
Akizungumzia haki ya wananchi kutoa maoni yao, Katambi alisema Serikali ipo tayari kupokea hoja za msingi kupitia njia za mazungumzo badala ya maandamano au vitendo vya vurugu.
"Kama kuna hoja ya msingi, watu waje wazungumze nami. Nitasimama kama Serikali kupokea hoja hizo. Hadi sasa hakuna hoja yoyote ambayo Serikali imeshindwa kuitolea majibu," alisisitiza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...