Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni Dodoma
Serikali imeonyesha utayari wa kuangalia uwezekano wa mashindano ya Ligi ya Muungano kuanza kuchezwa pia Tanzania Bara, hatua inayolenga kuimarisha ushiriki wa pande zote mbili za Muungano na kukuza maendeleo ya michezo nchini.
Hoja hiyo iliibuliwa bungeni leo na Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi, ambaye alihoji sababu za mashindano hayo kuendelea kufanyika Zanzibar pekee kwa muda mrefu na kusisitiza umuhimu wa kuyapanua ili yajumuishe Tanzania Bara.
Akichangia mjadala huo, Shangazi alisema kuwa kuchezwa kwa mashindano hayo katika pande zote za Muungano kutasaidia kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuongeza ushindani wa michezo na kutoa fursa sawa kwa wanamichezo wa Bara na Visiwani.
Akijibu hoja hiyo kwa niaba ya Serikali, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamisi Mwinjuma, alisema hakuna sheria wala kanuni inayozuia Ligi ya Muungano kuchezwa Tanzania Bara, bali hali iliyopo kwa sasa ni matokeo ya mazoea yaliyojengeka kwa miaka mingi.
Mwinjuma alieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa na kufanyiwa maboresho kupitia mazungumzo na makubaliano ya wadau husika ili kuhakikisha mashindano hayo yanawanufaisha wananchi wa pande zote za Muungano.
“Serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana na wadau wa michezo kujadili uwezekano wa mashindano haya kufanyika pia Tanzania Bara endapo kutakuwa na makubaliano ya pamoja,” alisema.
Aidha, alibainisha kuwa moja ya sababu zilizochangia mashindano hayo kufanyika zaidi Zanzibar ni kutokana na ukweli kwamba Tanzania Bara tayari ina idadi kubwa ya ligi na mashindano mbalimbali ya soka, hivyo Zanzibar imekuwa ikipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa matukio hayo ili kuongeza shughuli za michezo visiwani.
Hatua hiyo ya Serikali imepokelewa kama ishara ya kufungua ukurasa mpya katika uendeshaji wa Ligi ya Muungano, huku wadau wa michezo wakitarajia kuona mashindano hayo yakipanuliwa zaidi ili kuleta usawa wa ushiriki na kuongeza chachu ya maendeleo ya soka katika pande zote za Muungano.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...