Na Victor Masangu,Kibaha

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba ameitaka jamii kuwawezesha kiuchumi vijana wa kiume ambao wamesahaulika.

Simba ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Kikundi cha Super Women 2017 na kuwa baada ya wanawake kufanikiwa vijana wakiume nao waangaliwe.

Amesema kuwa kwa muda mrefu jamii iliwekeza kudai haki za wanawake ambapo kwa sasa wamepiga hatua ya kimaendekeo baada ya nguvu kubwa kutumika huku wale wa kiume wakiwa wamesahaulika.

Naye mwanzilishi wa kikundi hicho Betty Msimbe amesema kuwa wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukopeshana fedha kwa riba nafuu kupitia mfuko wa kikundi kwa fedha wanazoweka ambapo mkopo ni mara tatu ya fedha waliojiwekea.

Kwa upande wake mwenyekiti kikundi hicho Betha Kimambo amesema kuwa wanatarajia kuanzisha mradi wa kukodisha vyombo ili kuongeza kipato ndani ya kikundi.

Naye mratibu wa kikundi hicho Maria Msimbe amesema kuwa wanahamasisha wanawake kujiunga ili kujikomboa kiuchumi.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...