HATIMAE wamesikia na Kukata kiu ya wapenzi watazamaji wa Filamu za kinaijeria ndivyo unaweza sema,Enzi za Ini edo ,aki na ukwa na wengine waliotikisa miaka ya nyuma kwa filamu za kutisha na kufundisha sasa utawaona ndani ya St Swahili.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes Limited David Malisa ameweka wazi kuwa kwa Mara ya Kwanza wapenzi wa Filamu za Kinaijeria kwa Watanzania watashuhudia filamu hizo ambazo zimewekewa sauti za kutafsiri kwa Lugha ya Kiswahili kuanzia Jumamosi mpaka Jumapili kuanzia Mwezi Juni mwaka huu.

Akiongeza zaidi kupitia Kampeni yao mpya "Tumejiamulia kukupa Raha" ikiwa na Lengo la kuwaweka karibu watazamaji wa King'amuzi hicho na kuwakaribisha wateja wao wapya kushuhudia maudhui mapya ya kiburudani zaidi kwa ofa kedekede kuanzia kushuka kwa bei ya vifurushi mpaka kununua King'amuzi chenyewe.

Hata hivyo amesema Filamu za Kibongo hazijaachwa nyuma hivyo ni bandika bandua na wanatarajia kuweka ingizo jipya la filamu za kibongo kama sehemu ya Kuendelea kuwapa sapoti Watayarishaji wa Kibongo kupitia chaneli ya St Swahili.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...