TAKUKURU Mkoa wa Geita imefikisha mahakamani watumishi 9 wa umma kwa tuhuma za kutumia vibaya na kuiba fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 89,055,107 na senti 50.
Watumishi hao walikamatwa baada ya uchunguzi wa TAKUKURU kubaini walikuwa wakifanya vitendo vya rushwa na ubadhirifu. Kati yao watumishi 3 wa Manispaa ya Geita walikuwa wakikusanya mapato ya Serikali kupitia mfumo wa LGRCS lakini walikwepa kutoa stakabadhi na kutumia mashine za POS. Pesa zote zilizokusanywa hazikufika Serikalini na jumla ya shilingi milioni 48,067,500 ilipotea.
Wengine 4 ni watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita ambao walirudishia fedha za Mahakama Kuu Masjala Ndogo Geita kisha wakazitaka tena kwa njia ya rushwa kupitia simu na miamala ya benki. Kiasi kilichotumika vibaya hapo ni shilingi milioni 41,987,607 na senti 50.
Watumishi wengine 2 kutoka Idara ya Utafit iwa Madawa Mwanza na Hospitali ya Rufaa Bugando pia walishirikiana nao. Baada ya kukamilisha uchunguzi na kupata vibili kutosha, washtakiwa wote wamefunguliwa mashtaka 4 mahakamani tarehe 17 Juni 2026 na kesi zao zinasikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.
Mkuu wa TAKUKURU Geita Ndugu Said Lipandaje amesema hatua hiyo inaonyesha Serikali imedhamiria kupambana na rushwa bila woga.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...