Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema Tanzania bado haina mgonjwa wa Ebola na imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha ulinzi dhidi ya ugonjwa huo pamoja na kusaidia juhudi za kikanda za kudhibiti maambukizi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nchi inabaki salama dhidi ya tishio la ugonjwa huo unaoendelea kuripotiwa katika baadhi ya nchi jirani.
Amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa vifaa kinga katika bohari za dawa, kusimika maabara mbili za ziada kwa ajili ya uchunguzi na upimaji wa wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na Ebola, pamoja na kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na uchunguzi katika maeneo yote ya mipakani na vituo vya kutolea huduma za afya.
Aidha, zaidi ya watu 45,000 wamefikiwa na mafunzo kuhusu njia za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, hatua inayolenga kuongeza uelewa wa jamii na kuimarisha utayari wa taifa kukabiliana na mlipuko wowote utakaoweza kujitokeza.
Waziri Mchengerwa amesema Tanzania imeendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za kikanda za kupambana na Ebola, akisisitiza kuwa usalama wa afya wa nchi jirani ni sehemu muhimu ya usalama wa afya wa Tanzania.
Amesema kupitia uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imeendelea kutoa ushirikiano kwa nchi jirani zilizoathirika na ugonjwa huo, ambapo tayari vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500 vimetolewa kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Pamoja na hatua hizo, Serikali imefafanua kuwa haijafunga mipaka yake, bali imeimarisha mifumo ya udhibiti, uchunguzi na ufuatiliaji katika maeneo yote ya kuingilia na kutoka nchini ili kuzuia kuingia kwa maambukizi.
Aidha, Waziri Mchengerwa amesisitiza kuwa mafanikio katika mapambano dhidi ya Ebola yanahitaji ushirikishwaji wa wadau wote, ikiwemo sekta binafsi, mashirika mbalimbali na wananchi kwa ujumla, kwani jukumu la kudhibiti ugonjwa huo haliwezi kubebwa na Serikali pekee.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...