Balozi wa Tanzania nchini China, Dkt. Suleiman Haji Suleiman, ameendelea na ziara yake inayolenga kukutana na wakuu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini China ikiwemo Chuo cha Hong Kong Polytechnic University (HKPU) ambapo amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa chuo hicho, Prof Daniel Shek.
Aidha, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa shule za Biashara, Sayansi na Uhandisi na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa kitaaluma kati ya Chuo cha Hong kong polytechnic na Chuo Kikuu cha Sayansi cha Nelson Mandela (NM-AIST) cha jijini Arusha nchini Tanzania.
Balozi Dkt. Haji amesema kupitia ushirikiano huo, HKPU imeonesha utayari wa kusaidia wanafunzi wa Tanzania kupata maarifa na uzoefu wa kimataifa katika maeneo ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI), Sayansi, Utafiti, Teknolojia na Uhandisi ambayo ndiyo nguzo muhimu za maendeleo katika dunia ya sasa pamoja na kutoa mafunzo kwa vitendo (Internship) kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
"Pamoja na mambo mengine, ushirikiano huu wa Tanzania na China katika Sekta ya Elimu, utahusisha programu maalumu za kukuza vipaji vya wanafunzi katika nyanja za Sayansi na Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, hatua ambayo itasaidia kuandaa kizazi chenye uwezo wa kushindana katika uchumi wa maarifa na ajira za kimataifa," amesema.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...