MERIDIANBET, kupitia programu yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imeendelea kuthibitisha kuwa mafanikio ya biashara yana maana zaidi yanapoweza kugusa maisha ya watu moja kwa moja. Safari hii, kampuni hiyo imefika katika kata ya Kasekese, Manispaa ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi na kutoa msaada wa taulo za kike katika kampeni ya Hedhi Salama, hatua ambayo imepokelewa kwa furaha kubwa na viongozi pamoja na wananchi wa eneo hilo. Msaada huo umebeba ujumbe mkubwa wa matumaini, heshima na uwekezaji katika kizazi cha kesho.
Kwa miaka mingi, changamoto ya upatikanaji wa bidhaa za msingi za usafi imekuwa ikiwakabili wasichana wengi, hasa katika maeneo ya vijijini. Kutokana na hali hiyo, baadhi yao hulazimika kukosa vipindi vya masomo au hata kuathiriwa kisaikolojia kutokana na mazingira yanayowazunguka. Meridianbet imeona umuhimu wa kushiriki katika kampeni hii ya Hedhi Salama hili kuhakikisha kuwa wasichana wanapata mahitaji muhimu yanayowasaidia kuendelea na masomo yao kwa kujiamini zaidi.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba na nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10#.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasekese Bi. Bahati Kasanga alieleza kuwa mchango huo umefika kwa wakati muafaka na utaongeza nguvu katika jitihada za kuhakikisha wasichana wanabaki shuleni na kufikia malengo yao ya kielimu. Alisisitiza kuwa msaada wa Meridianbet sio tu umetoa suluhisho la muda mfupi, bali pia umeleta hamasa mpya kwa jamii kuzungumza kwa uwazi kuhusu afya ya hedhi na haki za mtoto wa kike. Kauli hiyo imeungwa mkono na wadau mbalimbali ambao wamepongeza hatua ya kampuni hiyo kuwekeza katika maisha ya vijana.
Kwa upande wake, Meridianbet imeendelea kusisitiza kuwa dhamira yake ni kuwa zaidi ya kampuni ya burudani, ni kuwa mshirika wa maendeleo ya jamii. Kupitia miradi yake ya kijamii inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, kampuni hiyo imekuwa ikilenga kugusa maisha ya wananchi kwa njia zinazozalisha matokeo chanya ya muda mrefu. Msaada huu wa taulo za kike ni sehemu ya maono mapana ya kuhakikisha kuwa kila msichana anapata nafasi sawa ya kufanikiwa bila kuzuiwa na changamoto zinazoweza kutatulika.
Katika kipindi ambacho vijana ndio nguvu kazi na tumaini la taifa, Meridianbet inaamini kuwa kila hatua inayochukuliwa leo inaweza kubadilisha maisha ya kesho. Kupitia msaada huu kwa wasichana wa Wilaya ya Tanganyika, kampuni hiyo imeonyesha kuwa uwajibikaji kwa jamii sio kauli mbiu pekee, bali ni ahadi ya kweli ya kushiriki katika kujenga Tanzania yenye usawa, afya bora na fursa kwa kila kijana.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...