Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV

SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujiandaa mapema kukabiliana na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia yanayotarajiwa katika miaka 30 ijayo, ikieleza kuwa zaidi ya asilimia 70 ya shughuli za kiuchumi zitakuwa zikifanyika kwa njia za kidijitali.

Hayo ameyasema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Nsubili Joshua, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omary, wakati wa Kongamano la Miaka 30 ya TRA tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, lililoandaliwa na TRA kupitia Chuo cha Kodi.

Joshua alisema mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani yanahitaji TRA kuwa mbele ya wakati kwa kuandaa mifumo madhubuti ya usimamizi wa kodi itakayoweza kukusanya mapato kutoka biashara za mtandaoni na huduma zinazovuka mipaka ya nchi.

Alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 30 ya TRA, bado kuna haja ya kuimarisha mifumo ya kodi ili iendane na kasi ya maendeleo ya uchumi wa kidijitali unaotarajiwa kutawala katika miaka ijayo.

“Katika miaka 30 ijayo zaidi ya asilimia 70 ya shughuli za kiuchumi zitafanyika kwa njia za kidijitali hivyo TRA inapaswa kuwa tayari kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kwa ufanisi bila kuathiri mazingira ya biashara na ubunifu,” amesema Joshua.

Alifafanua kuwa lengo la Serikali si kuzuia maendeleo ya teknolojia, bali kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kodi na ulinzi wa mapato ya taifa huku mazingira bora ya uwekezaji na ushindani wa haki yakiendelea kudumishwa.

Aidha, aliitaka TRA kuongeza uwekezaji katika matumizi ya akili mnemba (AI), uchambuzi wa takwimu na mifumo ya ufuatiliaji wa miamala kwa wakati halisi ili kubaini mianya ya ukwepaji kodi na kuimarisha uwazi katika ukusanyaji wa mapato.

Joshua alisema matumizi ya teknolojia hizo yatasaidia kugundua udanganyifu mapema, kupunguza mawasiliano yasiyo ya lazima kati ya walipakodi na maafisa wa kodi pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.

Pia aliitaka TRA kuendelea kubuni mifumo rahisi ya usajili, ukadiriaji na ulipaji kodi kwa sekta isiyo rasmi ikiwemo wafanyabiashara wadogo na wakulima, ili kupanua wigo wa walipakodi na kuongeza mapato ya ndani.

Alisema mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yatategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa nchi kukusanya mapato ya ndani na kuyasimamia kwa ufanisi, jambo linaloifanya TRA kuwa na jukumu muhimu katika safari ya maendeleo ya taifa.

Joshua alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya TRA, wafanyabiashara, watafiti na wadau wengine wa kodi ni muhimu katika kujenga mfumo wa kodi unaoendana na mahitaji ya uchumi wa kisasa na kuhakikisha Tanzania inanufaika kikamilifu na mapinduzi ya teknolojia yanayoendelea duniani.
Kamishina Mkuu wa TRA CPA Yusuph Mwenda akitoa maelezo kuhusiana tangu kuanzishwa mamlaka ya Mapato katika kongamano la miaka 30 tangu Kuanzishwa lililofanyika Ukumbi wa Serena ,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Nsubili Jushua akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omary wakati akizindua Kongamano la Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato (TRA) lililofanyika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Kodi Profesa Isaya Jairo akizungumza kuhusiana na kuratibu Kongamano hilo kwa lengo kukutanisha wadau kujadiliana miaka 30 ijayo juu utendaji wa TRA.jijini Dar es Salaam.



Picha za pamoja za Makundi katika kongamano la TRA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...