Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Vijana nchini wametajwa kuwa nguzo muhimu katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya sekta ya kaboni, huku Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo wakihimizwa kuongeza fursa za ajira, mafunzo na ushiriki wao katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yameelezwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Kaboni Afrika (ACA) Kaley Milao katika kongamano la vijana lililofanyika Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa changamoto za tabianchi zinaweza kubadilishwa kuwa fursa za maendeleo, ubunifu na ajira kwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Amesema ACA imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha ushiriki wa vijana kwenye masuala ya mazingira kupitia mikutano na programu mbalimbali zinazolenga kujenga uelewa na uwezo wa kizazi kipya katika sekta ya kaboni na uhifadhi wa mazingira.

Kaley mafanikio yaliyopatikana, alisema kupitia kongamano la Green Youth Summit 2025, wanafunzi watano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipata ajira za muda mfupi huku mwanafunzi mmoja wa kike akipata ajira ya kudumu, hatua iliyolenga kuwawezesha vijana kitaaluma na kiuchumi.

Aidha amesema ACA imeendelea kutekeleza programu ya inayotumia michezo, elimu na ubunifu kuhamasisha watoto na vijana kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira, kwa lengo la kujenga kizazi chenye uelewa wa masuala ya mazingira tangu utotoni.

Katika kongamano hilo, ACA ilitoa wito kwa taasisi mbalimbali ikiwemo Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuongeza nafasi za ajira, mafunzo kwa vitendo na fursa nyingine kwa vijana ili kuimarisha uwezo wao wa kiuchumi na kitaaluma.

Mtendaji huyo alisema vijana wengi wana mawazo, ubunifu na nguvu kazi kubwa inayoweza kuchangia maendeleo ya taifa, lakini wanahitaji kuaminiwa, kupewa nafasi na kuwezeshwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

Aidha amesema ACA imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake katika kuimarisha agenda ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo limeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kujenga ushirikiano kati ya Serikali, taasisi za elimu, sekta binafsi na vijana katika kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa huku yakitoa fursa za maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Kaboni Afrika    (ACA) Kaley Milao  akizungumza katika kongamano la vijana lililofanyika Dar es Salaam kuhusiana na harakati ya Taasisi katika kuwainua vijana katika uhifadhi wa mazingira wa kupata kipato.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...