Na. Mtemi Sona

Dodoma. Mwenyekiti wa Ujenzi Sports Club, Arch. Ibrahim Chatila, amesema uongozi mpya umejipanga kuijenga timu hiyo kuwa ya kisasa, imara na yenye ushindani mkubwa katika mashindano yote itakayoshiriki.

Akizungumza kuhusu mikakati ya kuiboresha klabu hiyo iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, Chatila amesema lengo kuu ni kuunda kikosi chenye ubora wa hali ya juu kitakachokuwa na uwezo wa kushindana na timu mbalimbali nchini.

Amesema hatua za awali zitahusisha usajili wa wachezaji bora pamoja na kuimarisha benchi la ufundi kwa kuwashirikisha makocha wenye uwezo na sifa zinazohitajika ili kuongeza ushindani wa timu.

"Tunataka kuunda timu yenye wachezaji watakaoweza kuleta ushindi na ambao watazingatia weledi, nidhamu na taaluma katika kila mashindano tutakayoshiriki," amesema Chatila.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa uongozi mpya uliochaguliwa umeazimia kuijenga upya Ujenzi Sports Club kwa misingi ya umoja, utawala bora na uwajibikaji kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji hadi wanachama.

Kwa mujibu wa Chatila, mafanikio ya timu hayatategemea ubora wa kikosi pekee, bali pia uimara wa mifumo ya uendeshaji wa klabu.

Mbali na masuala ya kiufundi, amesema uongozi wake umeweka mkazo katika kuimarisha uchumi wa klabu kwa kutafuta wadhamini na wadau mbalimbali watakaosaidia kuiendesha timu kwa kiwango cha kisasa.

"Lengo letu ni kuwa na klabu inayojitegemea kiuchumi, yenye uwezo wa kujiendesha na kushiriki mashindano kwa ushindani mkubwa," amesema.

Arch. Ibrahim Chatila ni Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambayo ni moja ya taasisi zinazounda Ujenzi Sports Club. Pia ni kocha mwenye leseni ya CAF na amewahi kuwa mjumbe wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida kwa kipindi cha miaka minne.

Yeye ni miongoni mwa viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni kuiongoza Ujenzi Sports Club, klabu inayoundwa na taasisi 10 zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi.

Klabu hiyo hushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, riadha, kuvuta kamba na michezo mingine ya ushindani.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...