Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML), Dominick Marandu, amesema kampuni hiyo imeendelea kuwa kinara katika ushirikishwaji wa Watanzania kwenye sekta ya madini kupitia ajira, manunuzi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii, amesema GGML imekuwa mshiriki na mdhamini wa Jukwaa la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCCF) tangu lilipoanzishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 22, 2026, wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Tano la LCCF jijini Mwanza, Marandu amesema kampuni hiyo inaamini rasilimali za madini zinapaswa kuwanufaisha Watanzania pamoja na jamii zinazozunguka maeneo ya migodi, amesisitiza kuwa ushirikishwaji wa wananchi ni sehemu muhimu ya maendeleo ya sekta hiyo.

Amesema GGML imefanikiwa kuwaajiri Watanzania kwa kiwango kikubwa, ambapo asilimia 98 ya wafanyakazi wake ni wazawa wenye taaluma na ujuzi mbalimbali wanaoshiriki katika shughuli za uzalishaji, na hatua hiyo inalenga kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani na kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa.

Marandu pia ameeleza kuwa kampuni hiyo inaendelea kutoa kipaumbele kwa wazawa katika manunuzi, akibainisha kuwa asilimia 97 ya manunuzi yaliyofanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026 yalifanywa kupitia kampuni za Watanzania, ambapo GGML inafanya kazi kwa karibu na Tume ya Madini kuhakikisha sheria za maudhui ya ndani zinazingatiwa kikamilifu.

Aidha, kupitia programu ya Graduate, amesema zaidi ya wahitimu 300 wa vyuo vikuu wamenufaika katika kipindi cha miaka saba iliyopita kwa kupata mafunzo ya vitendo yanayowawezesha kupata uzoefu wa kazi, huku baadhi yao wakiajiriwa pindi nafasi zinapopatikana, aidha kampuni inaendelea kutekeleza takribani miradi 60 ya Uwajibikaji na urejeshaji kwa Jamii (CSR) katika maeneo yanayozunguka mgodi.

Marandu amewahimiza Watanzania, hususan vijana, kutumia fursa zinazotolewa na GGML kupitia ajira, mafunzo na utoaji wa huduma mbalimbali, amesema ushiriki wa wazawa katika sekta ya madini ni msingi wa kuongeza tija, kukuza uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...