Na FARIDA MANGUBE MOROGOGO
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kada ya Maendeleo ya Jamii inapaswa kuwa injini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuongoza mageuzi ya fikra, kuimarisha uchumi wa wananchi na kujenga jamii yenye maarifa, uzalishaji, ubunifu na uzalendo.
Ameyasema hayo Leo Julai 1 Mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vitengo vya Maendeleo ya Jamii ngazi ya mikoa, Dkt. Gwajima amesema mafanikio ya Dira ya 2050 hayatategemea ukubwa wa bajeti au idadi ya miradi ya maendeleo, bali uwezo wa kubadilisha fikra na tabia za Watanzania katika kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Waziri Gwajima amewataka wakuu wa vitengo vya maendeleo ya jamii kuhamasisha mapinduzi ya fikra yatakayojenga utamaduni wa kuthamini kazi, uzalishaji, ubunifu, matumizi ya teknolojia, uwajibikaji na kujitegemea. Aidha, alisema ni wakati wa kuifanya taaluma ya maendeleo ya jamii itumie mifumo ya kidijitali na taarifa zinazotokana na ushahidi ili kupanga na kutekeleza afua zenye matokeo yanayopimika kwa wananchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eliakim Maswi, amesema utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji mabadiliko makubwa katika sekta ya maendeleo ya jamii ili iweze kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.
Ameeleza kuwa pamoja na Serikali kuendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo, mafanikio yake yatategemea pia mabadiliko ya wananchi kupitia kazi ya maafisa wa maendeleo ya jamii.
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa Vitengo vya Maendeleo ya Jamii Tanzania Bara, Elis Simonile, amesema kikao hicho kimewapa fursa ya kujitathmini, kubaini changamoto na vikwazo vinavyoikabili kada hiyo pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji kwa lengo la kuleta mabadiliko ya tabia na kuimarisha uzalendo miongoni mwa wananchi.
Simonile amesema vitendea kazi walivyokabidhiwa vitasaidia kuongeza ufanisi wa kazi kwa kuwa awali uhaba wa vifaa ulikuwa kikwazo kikubwa katika kuwafikia wananchi. Aliongeza kuwa matumizi ya mifumo ya kidijitali yatawezesha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa sahihi, hivyo kurahisisha utoaji wa ujumbe na utekelezaji wa afua za maendeleo ya jamii kwa ufanisi zaidi.
Kikao kazi hicho kilichowakutanisha Wakuu wa Vitengo vya Maendeleo ya Jamii kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara kililenga kutathmini utekelezaji wa majukumu ya kada hiyo, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha mchango wake katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kikao hicho kilihitimishwa kwa ugawaji wa vitendea kazi, ikiwemo kompyuta mpakato kwa lengo la kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika ukusanyaji, uchambuzi na utoaji wa taarifa za maendeleo ya jamii kwa wakati.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...