NAJUA wengi wetu tunamfahamu Mwanasheria maarufu nchini Fatma Karume ambaye anajulikana zaidi kwa jina la Shangazi.
Shangazi ambaye pia ni mwanaharakati alikuwa mstari wa mbele katika kuikosoa Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa inaongozwa na Hayati Dk.John Magufuli.
Staili ya Shangazi katika kuikosoa Serikali uliwakwaza baadhi ya viongozi na hali hiyo ilisababisha kuingia kwenye changamoto mbalimbali katika shughuli zake za kisheria na za uwanaharakati.
Miongoni mwa changamoto ambazo Shangazi alizipitia ni pamoja na tukio la kupigwa bomu katika Ofisi za IMMMA Advocates ambapo Fatma Karume alikua Mshirika.
Wakati Fatma Karume a.k.a Shangazi anaendelea na harakati hizo alikuwa na Maria Sarungi na wawili hao walishiriki kufichua mengi ya Serikali ya Hayati John Magufuli.
Ndio waliofichua tuhuma za upotevu wa fedha Sh. Trilioni 1.5 trillion ambao Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)profesa Mussa Asad aliuandika kupitia ripoti yake.
Ripoti ya upotevu wa fedha hizo ukasababisha Profesa Asad kuondolewa kazini.Hivyo Dk.Magufuli akawa Rais wa kwanza tangu Uhuru kumfukuza CAG.
Fatma na Maria wakajipa kazi ya kuwa watetezi katika matukio yaliyokuwa yanatokea kwa mfano malalamiko ya watu kutekwa na wale waliokuwa wanaitwa wasiojulikana.
Waliotekwa kwa wakati ule walikuwepo pia kama kina Mo Dewji, Roma Mkatoliki, Mdude, Azory Gwanda.
Kwa wanaokumbuka vizuri baada ya Mama kuingia madarakani Shangazi aliamua kuwa mwanaharakati full time.Na wakati huo tayari Shangazi alikuwa amenyang’wanya kibali cha uwakili na IMMMA advocates walimtimua maana alikua hana muda wa kufanya kazi zao za uwakili.Kazi za uwanaharakati zilikua nyingi mno.
Hivyo katika awamu ya mama (Rais Dk.Samia) Shangazi na Maria walikua wameingia mfumo wa kulipwa fedha na NGOs kufanya uwanaharakati (Ford Foundation ikiwa moja wapo).
Hapo Fatma Karume alikubali hizo fedha lakini kumbuka alikua hana shida sana na hizo fedha kutokana na historia ya familia yake maana Babu yake Abeid Karume ndio aliyekuwa baba wa Taifa Zanzibar na baba yake akaja kuwa Rais wa Zanzibar.
Pia Shangazi bado alikuwa anapokea fedha za pango kwenye Jengo la IMMMA advocates, na pango za apartments alizojenga mume wake wa zamani ambazo wakagawana .Hivyo Shangazi hakuwa na dhiki ya fedha kama ilivyo kwa Maria.Kwa Maria yeye biashara inayomuweka mjini ni Uanaharakati.
Sasa Shangazi Fatma wakati nchi inaelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 akagundua biashara ya uanauharakati ina manufaa zaidi kwa watu ambao anawapigania kuliko manufaa yake.
Kuna makundi yaliyokuwa yametokea ndani ya CCM kuutaka Urais tulipokuwa tunaelekea 2025. Majina yaliyokuwa katika makundi kwa sasa tunayahifadhi kwa ile staili Nguruwe pita mkuki sina.
Katika uchaguzi ule mwaka 2025 baadhi ya waliokuwa ndani ya makundi kuutaka Urais walipanga na safu katika ngazi mbalimbali na hata kwa wabunge.
Harakati za hovyo na zisizo na tija kwa Taifa ndizo zilizosababisha na vurugu za Oktoba 29 mwaka 2025.Kupitia wanaharakati uchwara waliokuwa wanatumwa na wakubwa wao huko nje wakaja na Samia Must Go.
Hata hivyo wakati hayo yalipokuwa yakiendelea Shangazi aliona mwelekeo unavyoenda kuna damu zinakuja kumwajika kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.Waliokuwa wanatoa fedha kufadhili hayo yote akili yao iko kwenye madini na gesi iliyoko Lindi na Mtwara.
Kwa Shangazi wakati wote alikuwa anawaza na kuangalia kama ndio Samia Must Go halafu nani anachukua madaraka na kwa manufaa gani yeye mwenyewe akaogopa zaidi!!!
Shangazi akajitafakari na kuona anayoyafanya hayana tija kwake wala kwa Taifa lake hivyo aliamua kwenda Hija na alivyorudi akaamua kuachana na Uwanaharakati na mambo machafu yote ya Dunia.
Kwa sasa Shangazi ameamua kuishi maisha yqnayompendeza Mungu,amesimama katika misingi ya imani yake ya dini ya Kiislamu na anaendesha maisha katika utaratibu wenye utu, ubinadamu.Sio Shangazi yule aliyekuwa moto na page yake ilikuwa ya Faya.Leo amepoa Shangazi na maisha yanaendelea.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...