Na. Mwandishi wetu, DODOMA
Meneja wa Kanda Namba Sita, Lucas Nkelege amefungua rasmi kikao cha kwanza cha watumishi wa kanda kwa mwaka wa fedha 2026/2027, kilichofanyika kwa lengo la kuweka mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu na vipaumbele vya taasisi katika mwaka mpya wa fedha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, aliwataka watumishi kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji na ushirikiano ili kufanikisha malengo ya taasisi.
"Mwaka mpya wa fedha unapaswa kuwa mwanzo wa kuongeza ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yetu. Kila mtumishi ana wajibu wa kuhakikisha anatimiza majukumu yake kwa ufanisi na kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wananchi na wadau wetu," alisema Nkelege.
Aidha, aliwahimiza watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kufuata sheria, kanuni na taratibu za kazi, pamoja na kushirikiana katika kutekeleza mipango iliyowekwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Kikao hicho kilitoa fursa kwa watumishi kujadili vipaumbele vya mwaka mpya wa fedha, kuweka mikakati ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kuimarisha ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...