Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewataka wazazi na walezi kujinyima mahitaji mengine ili kuhakikisha watoto wao wanapata elimu, akisisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa mafanikio katika dunia ya sasa inayohitaji watu wenye ujuzi na maarifa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Julai 13, 2026 katika eneo la Chididimo, Kata ya Zuzu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Senyamule amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
Amesema Shule ya Sekondari Zuzu, ambayo awali ilikuwa ya mwisho kimkoa kwa ufaulu, sasa imepanda hadi nafasi ya tisa kimkoa, jambo alilolitaja kuwa ni mafanikio makubwa.
Amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa walimu, wazazi, wanafunzi na wadau wengine wa elimu, huku akisisitiza kuwa walimu hawawezi kufanikisha ufaulu bila wazazi kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo kila siku.
Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma umeendelea kufanya vizuri kitaifa katika elimu ya msingi kwa kushika nafasi ya pili, huku ukilenga kufikia nafasi ya kwanza kupitia ushirikiano wa karibu kati ya serikali, walimu na jamii.
Aidha, amewataka wazazi kuendelea kuiunga mkono serikali ambayo imewekeza katika ujenzi wa madarasa na miundombinu ya elimu, kwa kuhakikisha watoto hawakosi shule, amesema elimu si jambo la kusubiri bali ni uwekezaji unaoleta matokeo ndani ya muda mfupi.
Ameeleza kuwa watoto wanaopata elimu leo ndiyo watakaokuwa nguzo ya maendeleo ya vijiji, mitaa na kata katika miaka ijayo, kupitia maarifa na ujuzi watakaoupata shuleni.
Senyamule amesema zamani mtu aliweza kuishi bila elimu na akaendelea na maisha, lakini kwa kizazi cha sasa na kijacho hali hiyo haitakuwa rahisi kutokana na ongezeko la mahitaji ya wataalamu katika sekta mbalimbali, amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata elimu ili aweze kushindana na kukabiliana na mahitaji ya dunia ya kisasa.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...