Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa vyuo vikuu pamoja na shule za sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza Taaluma ya Uhasibu nchini.

Katika kuendeleza jitihada hizo, NBAA imetembelea Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam, tarehe 22 Julai 2026, ambapo ilitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu majukumu ya Bodi, fursa zinazopatikana katika Taaluma ya Uhasibu pamoja na taratibu za kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu waliosajiliwa.

Mafunzo hayo yaliwahusisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha (Bachelor of Accounting and Finance – BAF). Kupitia mafunzo hayo, wanafunzi walipata uelewa kuhusu nafasi ya NBAA katika kusimamia na kuendeleza Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu nchini, pamoja na umuhimu wa kuzingatia maadili, weledi na maendeleo endelevu ya Taaluma.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, CPA Nicholaus Kishamba, Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam, aliwahimiza wanafunzi kutumia vyema fursa ya elimu wanayoipata chuoni kwa kujiandaa kuwa wataalamu wenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya, amesema ziara hiyo imekuwa chachu kwa wanafunzi kwani imewapa fursa ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu NBAA, ikiwemo majukumu yake ya kisheria, huduma zinazotolewa na Bodi, taratibu za usajili wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu, namna ya kufanya mitihani ya Bodi pamoja na fursa za maendeleo ya Taaluma.

Amesema elimu hiyo inalenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa mapema kuhusu Taaluma ya Uhasibu na kuwaandaa kukidhi mahitaji ya soko la ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Ziara hiyo pia ilitoa nafasi kwa wanafunzi kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu Taaluma ya Uhasibu, ambapo walihimizwa kujifunza kwa bidii, kuzingatia maadili ya Taaluma na kujiendeleza kitaaluma ili kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu wenye ushindani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akizungumzia kuhusu dhamira ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha (Bachelor of Accounting and Finance – BAF) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe , Kampasi ya Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa NBAA Salim Kasumari akitoa elimu kuhusu namna ya kufanya mitihani ya Bodi kwa wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe , Kampasi ya Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa NBAA Happiness Mwamwembe akitoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe , Kampasi ya Dar es Salaam.
CPA Nicholaus Kishamba, Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam akitoa neno la shukrani kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuendelea kutoa elimu katika chuo hicho.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha (Bachelor of Accounting and Finance – BAF) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe , Kampasi ya Dar es Salaam wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na watumishi wa NBAA waliofika chuoni hapo kutoa elimu.
Baadhi ya watumishi wa NBAA pamoja na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe , Kampasi ya Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...