Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameitaka Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) kuhakikisha maazimio na matamko yanayopitishwa katika mikutano yake yanatekelezwa kupitia programu zenye manufaa ya moja kwa moja kwa nchi wanachama na wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo, tarehe 23 Julai 2026, alipokutana na Katibu Mkuu wa OACPS, Mhe. Moussa Saleh Batraki na ujumbe wake , waliofika Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu, usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari, uvuvi, uhifadhi wa mazingira ya bahari pamoja na kubadilishana uzoefu na teknolojia miongoni mwa nchi wanachama.

Ameeleza kuwa Zanzibar imeendelea kunufaika na programu mbalimbali zinazotekelezwa kupitia ushirikiano wa OACPS na Umoja wa Ulaya, zikiwemo programu zinazowawezesha wakulima wadogo kuboresha uzalishaji, kufikia viwango vya masoko na kuongeza ushindani wa mazao yao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa OACPS, Mhe. Moussa Saleh Batraki, ameishukuru Tanzania kwa mchango wake katika shughuli za Jumuiya hiyo na kupongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendeleza ajenda ya Uchumi wa Buluu. 

Halikadhalika, amesisitiza dhamira ya OACPS kuendelea kushirikiana na nchi wanachama katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazokabili Mataifa Madogo ya Visiwa na kuimarisha maendeleo endelevu. 










Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...