Na Janeth Raphael - MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa mawasiliano ya Serikali yanapaswa kuwa ya kimkakati, yenye uratibu na yanayozingatia weledi ili kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali pamoja na kulinda maslahi ya Taifa.
Rais Samia ametoa msisitizo huo leo Julai 28, 2026, wakati akifungua Semina Elekezi ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu Umuhimu wa Mawasiliano Serikalini, iliyofanyika Ikulu ya Tunguu, Zanzibar.
Semina hiyo ya siku mbili imewakutanisha kwa mara ya kwanza viongozi waandamizi kutoka Serikali zote mbili za Muungano kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu namna bora ya kuwasiliana na wananchi, kuhakikisha taarifa za Serikali zinatolewa kwa usahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Rais Samia amesema mawasiliano si jambo la ziada katika utendaji wa Serikali, bali ni sehemu muhimu ya uongozi na nyenzo ya kimkakati inayochangia mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
“Mawasiliano ni sehemu ya uongozi na nyenzo ya kimkakati ya kulinda maslahi ya Taifa,” amesema Rais Samia.
Ameeleza kuwa mawasiliano yenye ufanisi huongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo, hujenga uaminifu kwa Serikali na kuwapa wananchi fursa ya kuelewa sera, mipango na hatua mbalimbali zinazochukuliwa kwa manufaa yao.
Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa taarifa za Serikali zinapaswa kutolewa kwa wakati, kwa lugha rahisi kueleweka na kuzingatia takwimu zilizothibitishwa ili kuondoa upotoshaji wa taarifa na kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeendelea kupata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu, nishati na maeneo mengine ya maendeleo, hivyo kuna umuhimu wa kuyawasilisha mafanikio hayo kwa wananchi kwa ufasaha na kwa njia zinazofikia makundi mbalimbali.
Akizungumzia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Rais Samia amesema Serikali zote mbili tayari zimeanza kutekeleza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuboresha huduma zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Amebainisha kuwa takribani asilimia 70 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unategemea ushiriki wa sekta binafsi, hivyo mafanikio ya dira hiyo yatahitaji mawasiliano madhubuti pamoja na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi.
Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, amesema semina hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia ya kuwajengea viongozi wa Serikali uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi na wananchi.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha viongozi kuboresha utoaji wa taarifa kwa usahihi na kwa wakati, pamoja na kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika kuhabarisha umma kuhusu shughuli na mafanikio ya Serikali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...