Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Daniel Francisco Chapo amewasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu, kuanzia Julai 2 -4 , 2026.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Mheshimiwa Rais Daniel Francisco Chapo alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) ambaye aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Chapo atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mheshimiwa Rais Chapo atafungua rasmi Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam; atamtembelea Mama Maria Nyerere kwa lengo la kumsalimia na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ubalozi wa Msumbiji jijini Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa, ziara hii ni ya tatu kwa Mheshimiwa Chapo kufanyika hapa nchini tangu alipoingia madarakani mwaka 2024 jambo lililoakisi dhamira ya viongozi wa nchi hizi mbili ya kuendelea kuimarisha mahusiano ya kirafiki na ushirikiano wa uhusiano wa kindugu kati ya Tanzania na inatarajiwa kufungua fursa mpya za ushirikiano wa karibu yaliyojengwa juu ya historia ya ujirani mwema na mshikamano wa muda mrefu.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...