Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imesema watu 300,000 nchini wanatumia dawa za kulevya aina ya Heroin na kati yao 30,000 wanatumia dawa hizo kwa njia ya kujidunga.
Akizungumza katika semina kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuwajengea uelewa, Kamishna wa Kinga na Tiba Dk.Peter Mfisi amesema kwa mujibu wa taarifa ya hali ya dawa za kulevya mwaka 2023 inaonesha watu 300,000 wanatumia Heroin.
“Kati yao watu 30,000 wanatumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga.Maambukizi ya UKIMWI miongoni mwa wanaojidunga yalikuwa asilimia 36,maambukizi ya homa ya Ini asilimia 60,maambukizi ya kifua kikuu asilimia 11 wakati katika jamii yalikuwa asilimia 0.2.”
Kuhusu madhara ya kiuchumi yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya ,Dk.Mfisi amesema hudhoofisha afya ya mtumiaji hivyo kuathiri uwezo wa kufanya kazi,kutumika kwa rasilimali za taifa katika kuwatibu waraibu na kudhibiti dawahizo
Madhara mengine husababisha mzunguko haramu wa fedha kunakochangia mfumuko wa bei, kuhodhiwa kwa uchumi na wachache, ongezeko la pengo la vipato, kuwepo kwa uwekezaji haramu na utakatishaji fedha.Pia kukithiri kwa rushwa, umasikini kwa familia, jamii na taifa.
Akizungumzia makundi ya dawa za kulevya ameyataja ni Vichangamshi (Stimulants) ambapo huongeza kasi ya utendaji wa mfumo wa fahamu hivyo kuongeza mapigo ya moyo na kasi ya kupumua.Mfano: cocaine na mirungi.
Pia kuna Vipumbaza (Depressants): Hupunguza kasi ya utendaji wa mfumo wa fahamu hivyo kushusha mapigo ya moyo, kasi ya kupumua o Mfano: heroin, valium.
Kundi jingine la dawa za kulevya ni Vileta Njozi (Hallucinogens)ambapo husababisha mtumiaji kuhisi, kuona au kusikia vitu visivyokuwepo au tofauti na uhalisia. Mfano: bangi.
Wakati kundi lingine ni Bangi ambayo hutumika zaidi nchini ikifuatiwa na heroin, mirungi, cocaine na dawa tiba zenye asili ya kulevya.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...