Na Pamela Mollel,Arusha
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani kupitia GIZ imezindua awamu ya pili ya mpango wa Akili Bandia unaolenga kuwajengea uwezo wananchi kutumia teknolojia ya AI katika kutatua changamoto mbalimbali na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayesimamia Miundombinu, Uzalishaji, Jamii na Siasa, Mhe. Aguer Ariik Malueth, amesema mpango huo ni sehemu ya juhudi za Jumuiya kuwaandaa vijana, watafiti na wajasiriamali kutumia fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia ya Akili Bandia
Amesema awamu hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya wananchi 20,000 kutoka nchi wanachama wa EAC kupitia mafunzo ya AI, huku ikiweka mkazo katika kukuza vipaji, ubunifu na utafiti ili Afrika Mashariki iweze kujenga uwezo wa ndani na kushindana katika uchumi wa kidijitali duniani
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Afrika Mashariki na Kati katika BMZ, Joachim Schmitt, amesema Ujerumani inaona umuhimu wa nchi za EAC kuwa na mwelekeo wa pamoja katika maendeleo ya teknolojia ya AI, akibainisha kuwa uwekezaji mkubwa uliofanyika barani Afrika bado haujasambaa kwa usawa katika nchi zote
Naye Mkurugenzi wa Uvumbuzi na Teknolojia wa Kundi la Equity, Winnie Mangeni, amesema ushirikiano huo utatoa nafasi kwa wanafunzi, watafiti na wabunifu kutengeneza suluhisho zinazotumia AI katika sekta ya fedha na maeneo mengine yenye umuhimu kwa maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki
Katika hatua nyingine, waandaaji wametenga Dola za Marekani 50,000 kwa ajili ya kuzisaidia timu zitakazofanya vizuri katika shindano hilo, huku mwaka huu kukiwa na kipengele maalum kinachowaalika wabunifu kutumia AI katika kusaidia kugundua, kuzuia na kukabiliana na milipuko ya magonjwa, ikiwemo Ebola
Mpango huo pia unalenga kuimarisha ufundishaji na utafiti katika vyuo vikuu, kuongeza ujuzi wa kidijitali na kusaidia nchi wanachama kujenga sera zinazofanana kuhusu matumizi ya Akili Bandia, huku ukizingatia usawa wa kijinsia na kuhakikisha teknolojia hiyo inawanufaisha wananchi kwa upana zaidi.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...