Na MWANDISHI WETU

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani,  imeunda kamati  maalumu itakayo saidia kukuza sekta ya uwekezaji  ikiwa ni hatua ya kuongeza mapato kupitia sekta hiyo.

Kamati hiyo inayoundwa na watu sita  imetangazwa leo katika Mkutano wa Robo ya Kwanza  ya Mwaka  wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Aidan Kitare, ameitaka kamati hiyo kufanya kazi kwa weredi, kuhakikisha  Kisarawe inapaa katika sekta ya uwekezaji , kuinua mapato  na kubuni vyanzo vipya vya  ukusanyaji mapato hayo.

Kitare amesema,  kutokana na usimamizi imara  wa vyanzo vya mapato  halmashauri hiyo inazidi kukua kwa kasi katika ukusanyaji ambapo ndani ya mwezi mmoja tu imekusanya zaidi ya sh. milioni 700 kutoka vyanzo vyake mbalimbali. 

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Nyahori Mahumbwe, amesema kamati hiyo itaongozwa na mwenyekiti wake Wakili Alkard Machumu,  ambaye pia ni Ofisa Ardhi wa halmashauri hiyo na Katibu atakuwa Joakim  Costa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji Idara ya  Maendeleo Biashara Viwanda wa halmashauri hiyo. 

"Dar es Salaam sasa imejaa fursa  za uwekezaji zipo  mkoani   Pwani.  Hivyo tunalazimika sasa kupokea wawekezaji wengi wanaotaka kuwekeza hapa Kisarawe. Tunajiandaa kupokea wawekezaji hao  kwa  kuunda kamati  hii  ya uwekezaji,"amesema Mahumbwe. 

Amesema kamati hiyo  inawajibu wa kuandaa maeneo  muhimu ya uwekezaji ambayo  wawekezaji wanaweza kuwekeza bila kupata changamoto.

"Kwa mantiki hiyo kama kuna maeneo ya uwekezaji  basi yanahusisha ardhi.  Ardhi iwe imepimwa na kuthaminiwa. Tuhakikishe maeneo hayo hayana utata kwa wawekezaji. Ni aibu  mwekezaji anawekeza kisha mwananchi anamshtaki mwekezaji,"amesema.

Amebainisha baada ya uundwaji wa kamati hiyo, kitaundwa kituo cha pamoja 'One Stop Centre'  ya Kisarawe  kurahisisha uwekezaji.

Amesema kituo hicho  kitahusisha  watalaamu wote  kutoka  taasisi zinazoguswa na masuala yanayo hususu  uwekezaji.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo  Wakili Machumu, amesema  kamati yake  itajikita kuangazia fursa za uwekezaji katika viwanda, utalii, hoteli, kilimo, ufugaji, michezo, burudani na elimu. 

" Pia  tutaanzisha Media kwa maana ya  kituo cha  radio na runinga. Wenzetu  halmashauri nyingi wameanzisha  na wamefika mbali,"amesema.

Amesma kamati imejiandaa kutembelea maeneo yote muhimu katika kata zote za wilaya ya Kisarawe kubaini fursa zilizopo.

"Uwekezaji mwingine ni katika maeneo kando ya misitu  ambako tutajikita katika  uwekezaji wa hoteli  za kitalii, ujenzi wa ukumbi  wa kisasa wa mikutano  kituo cha mabasi .










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...