LEO Liverpool watapambana na Nottingham Forest kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Anfield, katika mechi itakayokuwa ya kwanza ya nyumbani kwa kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola.

Hii itakuwa mechi ya kwanza ya msimu wa 2026-27 kwenye dimba la Anfield, huku Liverpool wakitaka kurejea baada ya sare waliyopata siku ya kwanza dhidi ya Newcastle. Iraola, aliyekuwa akiongoza Bournemouth msimu uliopita, sasa ana jukumu zito la kuwarudisha "The Reds" kwenye ushindani wa ubingwa.

Liverpool walianzaa msimu huu wakiwa na matokeo ya kusisimua dhidi ya Newcastle, ambapo walifunga mabao mara mbili baada ya kuwa nyuma, kwa mabao ya Cody Gakpo na penalti ya Dominik Szoboszlai dakika ya 99, hivyo kupata sare ya 2-2.

Kwa upande wa Forest, msimu wao ulianza vibaya zaidi chini ya kocha mpya Oliver Glasner, baada ya kufungwa 1-0 nyumbani na Leeds United, ambao walipata ushindi kwa freekick ya moja kwa moja ya Anton Stach. Kwenye msimamo wa ligi kwa sasa, Liverpool wako nafasi ya 10 na pointi 1, huku Forest wakiwa chini zaidi, nafasi ya 15 bila pointi.

Kuhusu majeraha, Liverpool watakosa wachezaji kadhaa muhimu. Watakuwa bila Conor Bradley, Hugo Ekitiké, Joe Gomez, Jayden Danns na Giovanni Leoni kutokana na majeraha, huku Curtis Jones akiwa na tatizo la kiuno linaloweza kumzuia kucheza.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hata hivyo, silaha kuu ya Liverpool bado ipo Florian Wirtz anabaki kuwa tishio kuu la mbele, akisaidiwa na Federico Chiesa na Alexander Isak. Kwa upande wa Forest, hali ni nzuri zaidi kwani Glasner ana karibu wachezaji wote wanaopatikana, isipokuwa Nicolo Savona na Ryan Yates, hivyo timu yake itakuwa na nguvu kamili ya mashambulizi kupitia Ola Aina, Morgan Gibbs-White na Igor Jesus.

Historia ya mechi hizi mbili inaonyesha ushindani mkubwa. Katika mechi tano za mwisho kati ya timu hizi, Liverpool wameshinda mara tatu, Forest mara moja, na mechi moja imeishia sare.

Hata hivyo, kumbukumbu za hivi karibuni si nzuri sana kwa Liverpool msimu uliopita Forest walishinda 3-0 dhidi ya Liverpool kwa bao la Morgan Gibbs-White, kabla ya Liverpool kulipiza kisasi Februari 2026 kwa ushindi wa 1-0 uwanjani kwa Forest. Hii inaonyesha kuwa Forest si timu ya kudharauliwa, hata dhidi ya mabingwa wa zamani wa Ulaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...