Na Vero Ignatus, Michuzi TV Arusha
Maonesho ya siku kuu ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kaskazini yamehitimishwa mkoani Arusha, yakihudhuriwa na zaidi ya wananchi 100,000 na kushirikisha waonyeshaji 446 kutoka sekta mbalimbali. Maonesho hayo yaliyojikita katika kuonesha fursa, teknolojia na ubunifu katika kilimo, ufugaji na uvuvi, yamebeba kaulimbiu isemayo “Tambua Soko, Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050.”
Akizungumza wakati wa kufunga maonesho hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, aliwataka wakulima, wafugaji na wavuvi kutumia matokeo ya tafiti, teknolojia na zana bora za uzalishaji ili kuongeza tija. Aidha, aliwahimiza wakulima kutumia mbegu zilizoidhinishwa na kuzingatia kalenda ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza katika kilimo.
Makala alisema wakati umefika kwa wakulima kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa, ikiwemo kilimo cha umwagiliaji, huduma za ugani zinazotolewa kwa njia ya TEHAMA pamoja na mifumo ya kidijitali inayowawezesha kupata taarifa za hali ya hewa, masoko, pembejeo na huduma za kifedha kwa wakati. Alisema upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu bei za mazao katika masoko mbalimbali humsaidia mkulima kufanya maamuzi sahihi kuhusu mahali pa kuuza mazao yake na kupata bei yenye tija.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, alisema wakulima hawawezi kuongeza uzalishaji na kufikia hatua kubwa za maendeleo bila kutumia teknolojia za kisasa, zana bora za kilimo na pembejeo sahihi. Alisema Tanzania imejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, hivyo wakulima, wafugaji na wavuvi wanapaswa kutumia rasilimali hizo kwa tija huku wakizingatia matumizi ya teknolojia na mbinu bora za uzalishaji.
Babu pia alisema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa utaratibu wa ruzuku, hivyo akawataka kutumia fursa hiyo kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kufika katika maeneo yanayotambuliwa na Serikali.
Aliongeza kuwa iwapo mbegu zinazofanyiwa majaribio zitathibitishwa na wataalamu, zitakuwa fursa muhimu kwa wakulima kuongeza mavuno kwa eneo na hivyo kuongeza kipato. Alisisitiza kuwa matumizi sahihi ya teknolojia, mbegu bora na pembejeo yanaweza kuongeza tija na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Awali, akitoa salamu na kusoma taarifa ya maandalizi ya maonesho hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Maryam Ahmed, alisema kamati ya maandalizi ilifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha maonesho hayo yanafikia wadau wengi.
Alisema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuimarisha uhamasishaji na utoaji wa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, hatua iliyosaidia kuwafikia wananchi na wadau mbalimbali na kuongeza ushiriki katika maonesho hayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...