Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau mbalimbali katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuhifadhi mazingira, kukuza utalii na kuendeleza ubunifu wa vijana, ikieleza kuwa maeneo hayo ni sehemu muhimu ya kujenga uchumi endelevu na wenye fursa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Dhamira hiyo imebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Theobald Sabi, wakati wa hafla maalum ya mnada wa sanaa za picha iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika Hoteli ya Kwanza, Kizimkazi, Zanzibar.
Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Mwanamke Initiative Foundation (MIF) kwa kushirikiana na kampuni ya ubunifu ya Waba Group, ilihusisha mnada wa picha zilizopigwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, zikionesha mandhari, utamaduni, maisha ya jamii, utalii na urithi wa asili wa visiwa hivyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia aliwataka wadau wanaojihusisha na sanaa ya upigaji picha, hususan vijana, kutumia ubunifu wao zaidi katika kutangaza utalii wa Tanzania, akibainisha kuwa sekta hiyo ina fursa kubwa za kibiashara na inaweza kuwa chanzo muhimu cha ajira na kipato.
“Zaidi nawapongeza sana vijana walioshiriki katika upigaji wa picha hizi kwa ubunifu na uwezo wao wa kutumia picha kusimulia uzuri, utamaduni na maisha ya Tanzania. Kazi zao hizi zinaweza kuwa sehemu muhimu ya kutangaza nchi na pia kuwa chanzo cha mapato,” alisema Rais Samia.
Rais Samia pia alieleza kuvutiwa na ubunifu wa wapiga picha walioshiriki, akitaja miongoni mwa kazi zilizomvutia picha za pomboo (Dolphin) chini ya bahari, wanawake wenye asili ya Pwani wakilima mwani pamoja na mandhari mbalimbali za Zanzibar.
“Picha hizi zimenifurahisha sana kwa sababu zinatangaza mandhari za Zanzibar, utalii, utamaduni, mila na desturi zetu,” alisema.
Aidha, Rais Samia aliwashukuru wadau walioshiriki katika kufanikisha hafla hiyo, ikiwemo benki ya NBC ambayo ilikuwa miongoni mwa wadhamini muhimu wa tukio hilo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mwanamke Initiative Foundation, Bi. Wanu Hafidh Ameir (Mb), alisema fedha zitakazopatikana kupitia mnada huo zitaelekezwa katika kuunga mkono jitihada za kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia, kupunguza utegemezi wa nishati zinazochangia ukataji wa misitu na hivyo kusaidia uhifadhi wa mazingira na bioanuwai.
“Sanaa na mazingira ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba. Tunaweza kutumia sanaa katika kuhamasisha na kukusanya fedha kwa ajili ya kutunza mazingira. Fedha zitakazopatikana katika mnada huu zitasaidia harakati za upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, kulinda mazingira na kutangaza utalii,” alisema Bi. Wanu.
Akizungumzia nafasi ya NBC katika kuunga mkono agenda ya nishati safi ya kupikia, Sabi alisema benki hiyo iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwezesha mnyororo mzima wa nishati hiyo, kuanzia uzalishaji hadi matumizi.
“Sisi NBC, mtazamo wetu ni kufadhili mnyororo mzima wa nishati safi ya kupikia. Kwetu sisi huu ni zaidi ya ushiriki—ni sehemu ya dhamira yetu ya kujenga jamii endelevu, kulinda mazingira na kuunga mkono ubunifu unaobeba suluhisho kwa kizazi cha sasa na kijacho,” alisema Sabi.
Sabi aliongeza kuwa NBC inaona fursa kubwa katika sekta ya sanaa za picha, akisema picha zina uwezo mkubwa wa kujenga na kusambaza simulizi kuhusu utamaduni, sanaa na utalii wa Tanzania.
Alisema uwekezaji katika sekta hiyo unaweza kuwa sehemu ya fursa za biashara za kisasa zenye uwezo wa kukua ndani na nje ya nchi, huku ukichangia kuitangaza Tanzania kama moja ya vivutio muhimu vya utalii duniani.
“Picha ina uwezo wa kusema mengi bila kutumia maneno mengi. Tunapoibua vipaji vya vijana na kuwawezesha kutumia sanaa ya picha, tunakuwa pia tumewekeza katika kuitangaza Tanzania, utamaduni wetu na fursa zetu za utalii kwa hadhira ya ndani na kimataifa,”
“Kwa NBC, ushiriki huo unaendelea kuakisi dhamira ya benki ya kutumia nguvu ya biashara, ubunifu na ushirikiano wa wadau kuchangia maendeleo endelevu, uhifadhi wa mazingira na ujenzi wa fursa mpya kwa vijana.” alisema Sabi.
Mbali na kushiriki katika hafla hiyo, NBC ilikuwa miongoni mwa wadhamini muhimu wa tukio hilo na ilitunukiwa tuzo maalum ya kutoka kwa Rais Samia ikiwa ni utambuzi wa mchango wake katika kufanikisha hafla hiyo na kuunga mkono ajenda ya maendeleo endelevu, ikiwemo jitihada za kukuza nishati safi ya kupikia na uhifadhi wa mazingira.
Hafla hiyo pia ilitoa jukwaa kwa vijana kuonesha vipaji vyao katika sanaa ya upigaji picha. Zaidi ya vijana 200 walihusika katika mchakato wa kushiriki katika mpango huo, huku kazi za wapiga picha 15 zikichaguliwa na jumla ya picha 10 zikifanikiwa kuuzwa kupitia mnada huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Theobald Sabi tuzo maalum ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maandalizi ya hafla maalum ya mnada wa sanaa za picha uliolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia, kupunguza utegemezi wa nishati zinazochangia ukataji wa misitu na hivyo kusaidia uhifadhi wa mazingira na bioanuwai kupitia taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF). Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Kwanza, Kizimkazi, Zanzibar jana.

Akizungumzia nafasi ya NBC katika kuunga mkono agenda ya nishati safi ya kupikia, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Theobald Sabi (alieshika mic) alisema benki hiyo iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwezesha mnyororo mzima wa nishati hiyo, kuanzia uzalishaji hadi matumizi.

Akiwa kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bw. Theobald Sabi alipata wasaa wa kubadilisha mawazo na viongozi pamoja na wadau mbalimbali.

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Bw. Elvis Ndunguru (katikati) alipata wasaa wa kubadilisha mawazo na viongozi pamoja na wadau mbalimbali.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC, Bw Godwin Semunyu (kushoto) akifuatilia hafla hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...