Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba leo tarehe 07/08/2026 amefungua mafunzo ya maafisa Elimu kata na wakuu wa shule 868Tanzania Bara kwa njia ya mtandao kupitia Darasa Janja (Smart class).

Akizungumza na washiriki Dkt. Komba amesema,  mafunzo hayo yamelenga utambuzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kumudu Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) na kutoa wito kwa washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia kwa makini ili kwenda kusimamia utekelezaji wake.

Ameendelea kusema, TET imejipanga vyema katika utoaji wa mafunzo mbalimbali ili kuwapa wasimamizi wa Elimu na walimu kuweza kupata maarifa yatakaosaidia katika utendaji wao ili kuendelea kuinua kiwango cha Elimu nchini. 

Aidha,  Dkt. Komba amewataka washiriki  kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan za kuboresha elimu nchini zinazoendana na uzinduzi wa mkakati wa KKK alioufanya mwaka 2025.

“Tumeona tutoe mafunzo haya kwanza kuanza nanyi viongozi ili tuweze kuwa katika ukurasa mmoja wa kuelewa mkakati  na kutekeleza dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 ambayo inasisitiza umuhimu wa kila mtoto wa Kitanzania anapata stadi za KKK kama msingi wa kila mtoto katika ushiriki wake katika ngazi  mbalimbali za elimu.”Amesema Dkt. Komba.

Hata hivyo Dkt. Komba ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekonolojia  na Ofisi ya Waziri Mkuu , TAMISEMI  kwa kuendelea kuhakikisha inatoa rasilimali fedha katika utekelezwaji wa majukumu mbalimbali ya kielemu.

Jumla ya washiriki  868 wameshiriki mafunzo hayo ya KKK, ambayo yanawezeshwa na  wataalamu wa TET  ambapo yanatarajiwa kuwafikia waratibu elimu wa kata  idadi ya 3000.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...