Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Lot Debruyne, katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Baada ya makabidhiano hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji, huku wakisisitiza umuhimu wa kukuza biashara na uwekezaji.
Akizungumza na Balozi Mteule huyo, Waziri Kombo amesema Tanzania inalenga kuhamisha mwelekeo wa ushirikiano kutoka katika utegemezi wa misaada na kuelekea katika biashara na uwekezaji wenye manufaa kwa pande zote.
Ametaja kilimo na umwagiliaji, uhamishaji wa maarifa na ujuzi, pamoja na upatikanaji wa mitambo na teknolojia za kisasa za kilimo kuwa miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa za ushirikiano.
Aidha, Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa kuongeza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji, akieleza kuwa ongezeko la watalii kupitia safari za moja kwa moja za Brussels Airlines kwenda Kilimanjaro na Zanzibar ni fursa muhimu ya kukuza sekta ya utalii.
Viongozi hao pia wamebainisha maeneo mengine ya ushirikiano, ikiwemo ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, nishati safi na jadidifu, nishati ya kupikia safi, mabadiliko ya kidijitali na afya.
Kwa upande mwingine, wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Bandari za Antwerpen nchini Ubelgiji na Dar es Salaam, pamoja na fursa za ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Ghent na taasisi za elimu nchini Tanzania katika kukuza matumizi na ufundishaji wa lugha ya Kiswahili.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...