Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2026. Bei ya petroli imeshuka kwa Shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa Shilingi 101 kwa lita. Bei hizo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 2 Septemba 2026, saa 6:01 usiku.
EWURA inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, ambapo mabadiliko ya bei yanaendelea kuathiriwa pamoja na mambo mengine na hali ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015, bei za mafuta zinaendelea kupangwa kwa kuzingatia mfumo wa soko. Wafanyabiashara wote wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zisizozidi bei elekezi, na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa EWURA kwa kituo chochote cha mafuta kitakachouza zaidi ya bei elekezi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...