Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño, huku ikiwataka wananchi kuchukua tahadhari mapema dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa katika msimu wa Vuli 2026/27.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa mpango huo.
Mpango huo umeandaliwa kufuatia utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Agosti 18, 2026, uliotabiri uwepo wa hali ya El Niño yenye nguvu katika msimu wa Vuli 2026/27.
Kwa mujibu wa Serikali, mpango huo unalenga kuimarisha utayari na kuhakikisha hatua za mapema zinachukuliwa katika kuzuia, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali ya kawaida baada ya kutokea kwa madhara yanayoweza kusababishwa na El Niño.
Miongoni mwa hatua zilizopangwa ni kukarabati na kuboresha miundombinu inayoweza kuathiriwa na mvua kubwa, ikiwemo barabara, madaraja, mitaro na reli, pamoja na kuhakikisha huduma muhimu za afya, elimu, maji, umeme na mawasiliano zinaendelea kupatikana katika maeneo hatarishi.
Aidha, Serikali imepanga kuimarisha akiba ya chakula, vifaa vya uokoaji na misaada ya kibinadamu, pamoja na kuandaa maeneo ya muda kwa ajili ya kuwahifadhi wananchi watakaoweza kuathiriwa na maafa.
Serikali imeeleza kuwa makadirio ya rasilimali zinazohitajika kutekeleza mpango huo kwa sekta zote yanafikia takribani Sh bilioni 730, wakati fedha zilizotengwa katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya shughuli hizo ni Sh bilioni 10.
Pamoja na maandalizi hayo, Serikali imewataka wananchi kutotumia mvua hizo kwa hofu pekee, bali pia kuzitumia kama fursa kwa shughuli za uzalishaji, ikiwemo kilimo, ufugaji, uvunaji wa maji na uvuvi.
Wananchi wametakiwa kutumia mbinu bora za kilimo, kuchagua mazao na mbegu zinazofaa kwa msimu wa Vuli, huku wakichukua tahadhari dhidi ya maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko, maporomoko ya ardhi na milipuko ya magonjwa.
Serikali pia imewataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa rasmi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA, kuondoka mapema katika maeneo hatarishi na kutoa taarifa kwa mamlaka husika mara maafa yanapotokea.
Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa Agosti 26, 2026 ilitoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa inayoweza kuathiriwa na mvua za El Niño kuhakikisha maandalizi yanafanyika mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Serikali imesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, mamlaka za mikoa na halmashauri pamoja na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha athari za El Niño zinadhibitiwa na fursa zinazotokana na mvua hizo zinatumika kwa shughuli za maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...