KIZIMKAZI, ZANZIBAR — Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Kundi la Hanspaul, Satbir Singh Hanspaul, amefika Kizimkazi, Zanzibar, kutoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake mpendwa, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Hanspaul amefika katika makazi ya Rais Samia yaliyopo Kizimkazi, ambapo ametoa pole kwa Rais pamoja na familia yake kufuatia msiba huo.
Katika salamu zake za pole, Hanspaul amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan mahali pema peponi, huku akimtakia Rais Samia pamoja na familia yake nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki cha maombolezo.


.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...