Na Mwandishi wetu
WAKATI Ligi ya Wahenga Supper Cup, ikiendelea kulindima katika hatua ya Nusu Fainali, Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kinyerez kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Mrema 'Wahenga' ameandaa tamasha kubwa linalofahamika kama Kinyerezi Day.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Naibu meya huyo , Salehe Manyonga, katika hafla ya kukabidhi jezi kwa timu za soka zilizoingia Nusu Fainali ya Ligi ya Wahenga Supper Cup inayoshirikisha timu kutoka katika Kata ya Kinyerezi.
Manyonga, amesema KInyerezi Day itafanyika Septemba 19 mwaka huu na ambapo itapigwa fainali ya Wahenga Supper Cup itakayo tanguliwa na mechi kabambe za utangulizi.
Amesema tamasha hilo litaanza asubuhi kwa kushirikisha vikundi vya Jogging, kisha, kuendelea kwa michezo mbalimbali hususan mechi ya soka baina ya watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
"Tamasha hili litakuwa kubwa, tutakuwa na wasanii wakubwa wa muziki, mechi za maveterani wa soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia na zawadi nyingi zitatolewa,"amesema Manyonga.
Amebainisha Kinyerezi Day limeandaliwa na Diwani John Mrema 'Wahenga' ili kuwaweka pamoja wananchi wa kata hiyo kupitia michezo na buridani.
"Diwani amekuwa akisikiliza mawazo na maono ya wananchi wake. Ligi ya Wahenga Supper Cup imewavuita watu karibu katika kujadili mambo muhimu ya maendeleo ya kata yetu ya Kinyerezi. Siku ya Kinyerezi Day patakucha kwelikweli,"amebainisha Manyonga.
Kuhusu ugawaji wa jezi kwa timu zilizoingia Nusu Fainali ya Wahenga Supper Cup, Manyonga amesema, Diwani John Mrema, ametoa kama zawadi nje ya zawadi za timu zitakao ingia katika fainali na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo .
"Kuna zawadi nyingine nyingi zitratolewa kwa mabingwa wa ligi hii zikiwemo jezi. Jezi tulizo kabidhi kwa timu zilizo ingia nusu fainali Diwani Wahenga ambaye ni mwandaaji na mdhamini kupitia Wahenga Alumium siyo sehemu za zawadi za mabingwa. Hizi ametoa kuzipa moyo timu hizi kufanya vizuri zaidi,"ameeleza Manyonga.
Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Kinyerezi Day Septemba 19 mwaka huu kwani hakutakuwa na kiingilio zaidi ya kupata burudani isiyo na kifani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...