Na MWANDISHI WETU, Zanzibar

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amewataka makada wa chama hicho kuwa na uelewa mpana wa Itikadi, misingi na historia ya CCM ili waweze kutoa ufafanuzi sahihi kwa wananchi.

Hemed ameyasema hayo leo, Septemba 26, 2026, wakati akifungua mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya wa CCM kwa awamu ya pili, yaliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Uongozi Dambwe, Tunguu, Zanzibar.

Amesema sera za CCM zinalenga kuleta maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi, hivyo ni muhimu kwa makada kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sera, misingi na historia ya chama hicho.

Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujifunza na kupata tija, ikiwemo kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazokikabili chama.

Aidha, Hemed amesema CCM inapotoa ahadi kwa wananchi, inaendelea kuzitekeleza kwa vitendo, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama wa chama.

Katika hatua nyingine, amewataka makada hao kujifunza kwa kina historia ya CCM na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu misingi na Itikadi ya chama ili waweze kueleza na kutetea kwa usahihi misimamo na sera zake wanapowahudumia wananchi.

Zaidi ya makada na wanachama 380 wa CCM kutoka mikoa mbalimbali ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara wanashiriki mafunzo hayo yanayolenga kuongeza uelewa kuhusu Itikadi na Uenezi, pamoja na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...