Na MWANDISHI WETU - DAR ES SALAAM
WAKAZI wa Kata ya Kisutu, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, wameendelea kuhamasisha kampeni ya usafi kwa kuanzisha shughuli za usafi katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtendeni, Kata ya Kisutu, Mustaquim Daruga, na imeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shina Namba 8, Tawi la Mtendeni, chini ya Mwenyekiti wake, Al Hajj Mahmood Amirali Walrji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Daruga amesema wananchi wa Kisutu hawataki uchafu na kwamba usafi umefanywa kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wa kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi.
“Mkuu wa Wilaya ya Ilala amesema mtu atakayejihusisha na uchafu atatozwa faini ya Sh300,000 hadi Sh milioni moja au kifungo cha jela. Adhabu hii si kwa ajili ya watu wasafi. Hii ni kwa wachafu. Sisi Kisutu ni wasafi, haitatuhusu. Wachafu wafungwe na wapigwe faini,” amesema Daruga.
Daruga ameipongeza CCM Shina Namba 8 kwa kuanzisha kampeni hiyo katika ngazi ya shina, akisema hatua hiyo inapaswa kuwa mfano kwa mashina mengine katika kuhamasisha usafi wa mazingira.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kisutu, Tousif Bhojani, amesema tayari kata hiyo imezindua kampeni ya usafi katika ngazi ya kata, hivyo hatua iliyochukuliwa na Shina Namba 8 ni mwendelezo wa kuhakikisha maeneo yote ya Kisutu yanakuwa safi.
“Sisi Kata ya Kisutu kila siku tutaendelea na usafi. Nawaomba wananchi wa Kisutu wazingatie usafi. Hii iwe mfano kwa mashina mengine. Tuonyeshe kwa vitendo kuitikia wito wa Rais wetu wa kuhakikisha jiji letu linakuwa safi,” amesema Bhojani.
Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kisutu, Multazar Daruga, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusisitiza umuhimu wa Jiji la Dar es Salaam kuwa safi, akisema Kisutu itaendelea kutekeleza maelekezo hayo.
“Hii kampeni ya usafi Kisutu tunaisisitiza, lakini kata zingine nazo ziendelee. Tutaanza ngazi ya kata, Mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye nchi nzima itakuwa safi,” amesema Multazar.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Shina Namba 8, Tawi la Mtendeni, Al Hajj Mahmood Amirali Walrji, amewashukuru wananchi, wadau na taasisi mbalimbali kwa kujitokeza kushiriki kampeni hiyo.
Amesema Shina Namba 8 linatambua na kuheshimu tamko la Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi.
Ameahidi kuwa shina hilo litaendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi na kuhamasisha wananchi kuhakikisha Kata nzima ya Kisutu inakuwa safi, kuanzia ngazi ya shina.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...