Na Karama Kenyunko Michuzi tv
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wanaume kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini mapema magonjwa mbalimbali, ikiwemo saratani ya tezi dume.
Kikwete amesema hayo wakati wa hafla ya kuhamasisha uelewa kuhusu saratani ya tezi dume iliyofanyika katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam, akieleza kuwa uchunguzi wa afya ni muhimu kwa kuwa baadhi ya magonjwa yanaweza kugundulika kabla hayajaanza kuleta madhara makubwa.

Amesema saratani ya tezi dume inaweza kufuatiliwa kwa vipimo vya afya, ikiwemo kipimo cha PSA, huku akisisitiza kuwa wanaume wanapaswa kusikiliza ushauri wa wataalamu wa afya na kuepuka taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kikwete ameeleza kuwa saratani hiyo inapogundulika katika hatua za awali, mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa wakati, tofauti na pale ugonjwa unapochelewa kugundulika na kusambaa katika maeneo mengine ya mwili.
Amesisitiza pia umuhimu wa wanaume kuwashirikisha wake zao katika masuala ya afya na kufanya maamuzi ya matibabu kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Kairuki, Dkt. Asser Mchomvu alisema asilimia 43.6 ya wagonjwa wa saratani ya tezi dume hufika wakiwa na Ugonjwa uliosambaa.

"Tumedhamiria kuboresha matibabu ya tezi dume hapa nchini hata tukadhubutu kuleta technojia hii mpya na ya Kisasa kuondoa uvimbe bila mwilini bila kufanya upasuaji yaan HIFU,"alisema.
Aidha Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu hospitalini hapo, Kokushubila Kairuki alisema katika maadhimisho hayo yaliyoanza Septemba 13, 2026 wanaume 250 walijitokeza kupata ushauri na kupima saratani ya tezi dume

"Mahudhurio yapo chini ukilinganisha na ukubwa wa tatizo, juhudi kubwa zinahitajika kuhamasisha wanaume kupima saratani ya tezi dume mara kwa mara," alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...