Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewapa jukumu makada wake 460 kutoka kanda tisa za kichama kusimamia maadili na Itikadi ya Chama, pamoja na kuchangia upatikanaji wa wanachama wapya katika wilaya mbalimbali nchini.
Makada hao wamepewa jukumu hilo kupitia mafunzo ya Itikadi, Uenezi na kuongeza wanachama wapya yanayoendelea katika Chuo cha UVCCM Ihemi, mkoani Iringa, kuanzia Septemba 15 hadi 21, 2026.
Badala ya mafunzo hayo kuishia darasani, CCM imewataka washiriki kuyageuza kuwa utekelezaji wa moja kwa moja katika maeneo yao kwa kuwafikia wanachama na wananchi, kutoa elimu sahihi kuhusu Chama na kushiriki katika ujenzi na uimarishaji wa CCM.
Akifungua mafunzo hayo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, amesema makada hao wanapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko yanayofanywa ndani ya Chama kwa kutumia maarifa wanayoyapata kupitia mafunzo hayo.
“Makada waliopata mafunzo haya wanapaswa kuyatumia kuwafikia wanachama ili kutoa elimu kwa usahihi,” amesema Wasira.
Amesema CCM ina historia ndefu na nafasi yake katika siasa za Tanzania inawataka makada kuelewa kwa kina misingi na Itikadi ya Chama na kuisimamia katika utekelezaji wa majukumu yao.
Wasira amesema jukumu la makada hao halipaswi kuishia katika kuongeza idadi ya wanachama pekee, bali linapaswa kwenda sambamba na kuhakikisha wanaojiunga na CCM wanaelewa misingi, Itikadi na wajibu wao ndani ya Chama.
Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amesema makada hao hawakuchaguliwa kwa bahati, bali walipitia mchakato wa usajili na usaili uliofanyika katika kanda zote tisa za kichama kabla ya kuanza mafunzo.
“Awamu hii ni ya kwanza na makada 460 wamepata mafunzo. Kabla ya kuanza mafunzo, kila kanda ilifanya usajili na usaili wa washiriki,” amesema Kihongosi.
Amesema mpango huo unalenga kujenga wataalamu wa mafunzo katika kila wilaya, watakaokuwa na uwezo wa kufikisha elimu ya Chama hadi katika ngazi za chini.
“Kinachojengwa katika mafunzo haya ni utekelezaji wa mfano wa kitaifa unaolenga kujenga wataalamu wa mafunzo katika kila wilaya,” amesema.
Kihongosi amesema miongoni mwa malengo makubwa ya mpango huo ni kuhakikisha kila wilaya inachangia kupata wanachama wapya 500.
“Lengo ni kusajili wanachama wapya 500 kila wilaya nchini. Washiriki wanapaswa kubeba yale watakayofundishwa na kuyafikisha kwa wananchi ili kuhakikisha wanapata elimu wanayoitarajia na kujenga Chama,” amesema.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema jukumu walilopewa ni kubwa, kwa kuwa linawataka kutokaa na elimu waliyoipata, bali kuifikisha kwa wanachama na wananchi katika maeneo yao.
“Tunatakiwa kuhakikisha elimu hii haibaki kwetu. Tukirejea kwenye maeneo yetu, tunapaswa kuwafikia wanachama na kuwaeleza kwa usahihi yale tuliyojifunza,” amesema Noel Chilaga.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM Taifa.

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...