Na Victor Masangu, Kibaha

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia chama cha mapoinduzi (CCM) Mariamu Ulega katika kuunga mkono juhudi za seriklai katika kuboresha sekta ya elimu ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 2 kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika shule ya msingi ya Mkoani B iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha hususan katika suala la ujenzi wa kujenga uzio.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza kwa mchepua wa kiingereza katika shule ya msingi Mkoani B Katibu wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Mkoa wa Pwani Aziza Hussein kwa niaba ya mgeni rasmi Mbunge wa viti maalumu Mariamu Ulega ambaye pia Mke wa Waziri wa Ujenzi Abdalah Ulega.

Katibu huyo huyo wa UWT Mkoa akitoa salamu za Mbunge huyo amebainisha kwamba anatambua umuhimu mkubwa wa suala zima la elimu hivyo ameamua kuchangia kiasi hicho cha shilingi milioni 2 ambazo zitaweza kusaidia katika mwendelezo wa ujenzi wa uzio katika shule hiyo ya msingi Mkoani B yenye mchepuo wa kiingereza.

"Nashukuru sana nimeweza kushiriki na kualikwa katika mahafali haya ya kwanza katika shule hii ya msingi mkoani B lakini mimi ni Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani lakini kwa leo nimepewa heshima ya kipekee kwa ajili ya kuweza kumwakilisha Mbunge wa viti maalumu mheshimiwa Mariamu Ulega ambaye yeye ndiye aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizi z amahafali,"amebainisha Katibu huyo.

Aidha katibu huyo ameongeza kwamba lengo kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu, wazazi pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kutoa sapoti na michango yao ambayo itaweza kusaidia katika kukuza sekta ya elimu sambamba na kuboresha zaidi miundombinu katika shule hiyo.

"Mbunge wenu wa viti maalumu mheshimiwa Mariam Ulega ameniagiza kuja kumwakilisha na amesema yupo pamoja nanyi na kwamba amesema kuwa anachangia kiasi cha shilingi milioni mbili na na kuelekeza kwamba fedha hizo zitumike katika kuboresha miundombinu ya ujenzi wa uzio ili watoto hao waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki na salama na kwamba ataendelea kuisaidia shule hiyo katika mambo mengine mbali mbali,"ameongeza Katibu huyo.

Katika hatua nyingine amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kuleta mabadiliko makubwa katika kutekelza miradi ya maendeleo hususan kuboresha sekta ya elimu ikiwemo ujenzi i wa madarasa pamoja na madawati.

Pia katibu huyo mbali na kutoa salamu za mheshimiwa Mbunge wa viti maalumu Mariamu Ulega amesema na wao kama uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani wameamua kuchangia kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni moja na jitihada za kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

Nao baadhi ya wazazi na walezi akiwemo Teodory Joseph pamoja na Joseph Ogutu wameipongeza serikali kwa kuweza kuboresha sekta ya elimu huku wakiiomba kuweka misingi madhubuti ya kuendelea kutenga shule nyingine na kuziingiza katika progamu hiyo ya kuwa na mchepuo wa masomo ya kiingereza.

Mahafali ya kwanza ya kwa mchepuo wa kiingereza katika shule ya Msingi Mkoani B iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani imeweza kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, wazazi na walezi pamoja na wadau wengine mbali mbali wa maendeleo katika sekta ya elimu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...