Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo Septemba 23, 2026, imekutana wagonjwa waliowahi kuugua saratani na kupona kabisa, kwa lengo la kuwapongeza , na kuwashukuru wadau wanaofanikisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Bi. Prissila Kinyamagoha ameiomba jamii kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara, akisisitiza kuwa saratani ikigundulika mapema inatibika na kupona kabisa huku akiwashukuru kwa dhati wazazi waliojitoa na kuwa wavumilivu katika kipindi chote cha matibabu ya watoto wao hadi kufikia hatua ya kupona, huku akibainisha kuwa ushuhuda wao unatoa matumaini mapya kwa jamii.
Aidha, uongozi wa hospitali hiyo umetoa shukrani za kipekee kwa wadau wote wanaoendelea kufadhili matibabu hayo, huku ukitoa wito kwa wafadhili zaidi kujitokeza kwani mahitaji bado ni makubwa na idadi ya wagonjwa wapya inaongezeka kila siku.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...