Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 leo Sep 1,26 Umeangazia mafanikio makubwa ya Sekta Binafsi Wilaya ya Bukoba Vijijini kupitia uwekezaji wa Kiwanda cha kuchakata Parachichi cha "BallyVado"
Hii ni katika kutambuai mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza sekta ya kilimo-biashara (agribusiness) mkoani humo, ambapo kilimo cha parachichi kimekuwa kikikua kwa kasi kubwa..
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg.Wazo M. Mwang'onda, ametoa pongezi za dhati kwa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Mzee Depson Balyagati kwa kuwa na maono ya mbali na kuthubutu kuwekeza mamilioni ya fedha katika miundombinu ya kisasa ya kuchakata matunda hayo.
Aidha Ndugu Mwang'onda amebainisha kuwa nchi inahitaji wawekezaji wazawa wenye uzalendo kama wa Mkurugenzi Mzee Depson Balyagati, ambao hawaangalii faida yao tu, bali wanaangalia jinsi ya kuwasaidia wakulima wadogo vijijini kupata soko la uhakika.Kwa upande wake,
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitanda hicho Mzee Dspson Balyagati( Mnec Mstaafu) amesema kuwa uamuzi wa kujenga kiwanda hicho ulitokana na kuguswa na changamoto ya wakulima wa Bukoba kuona mazao yao yakipotea kwa kukosa masoko baada ya kuvuna. Na kusisitiza kuwa kiwanda chake sasa kipo tayari kununua parachichi zote za kiwango cha soko la kimataifa.
Naye Mbunge wa Bukoba Vijijini, Dkt. Jasson Rweikiza, ambaye alimpongeza Mkurugenzi Balyagati kwa kuleta kiwanda hicho karibu na wananchi, akiahidi kuwa uongozi wa jimbo utaendelea kuhamasisha kilimo cha parachichi ili kiwanda kisikose malighafi wakati wote wa uzalishaji.
#BallyVadoOil #MwengeWaUhuru2026
#BokobaToTheWorld



.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...