Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali na taasisi za dini zina wajibu wa kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano, kukuza maadili mema na kuchangia ustawi wa wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 20 Septemba 2026, katika hafla ya kuwekwa wakfu na kumketisha kitini Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba kuwa Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Zanzibar, iliyofanyika  Kanisa Kuu la Kristo, Mkunazini Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Kanisa na taasisi nyingine za dini zina mchango mkubwa katika elimu, afya, malezi, ujenzi wa maadili na maendeleo ya jamii, akisisitiza kuwa tofauti za kiimani zinapaswa kuwa msingi wa kuheshimiana, kuvumiliana na kushirikiana katika kudumisha amani ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba na kumtakia hekima, afya, nguvu na neema ya Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza Dayosisi ya Zanzibar.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya kihistoria kwa lengo la kuhifadhi historia ya Zanzibar, kutoa elimu na kukuza utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Akizungumzia hali ya hewa, Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mvua za Vuli zinazotarajiwa kuathiriwa na hali ya El Niño, huku akizitaka taasisi za dini kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa.

Naye , Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano anaouonesha kwa taasisi za dini na juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi .




















Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...