REAL Sociedad watawakaribisha Celta Vigo katika uwanja wao wa Reale Arena mjini Donostia-San Sebastián, katika mechi ya ligi kuu ya uhispania Laliga na itakayovuta hisia za mashabiki wengi wa ligi kuu ya Uhispania msimu huu wa 2026/27.
Real Sociedad wameanza msimu kwa mtikisiko Fulani, Hadi kufikia raundi ya tatu ya ligi, timu hiyo ilishinda mechi dhidi ya RCD Espanyol kwa mabao 2-1, lakini bado ipo katika nafasi za chini ya msimamo kutokana na matokeo hafifu ya raundi za awali. Hali hii inaonyesha kuwa kocha wa Real Sociedad anahitaji kuimarisha ulinzi na mashambulizi ili timu iweze kupanda nafasi za juu za msimamo.
Kwa upande wa Celta Vigo, timu hiyo imeanza msimu vizuri zaidi ikilinganishwa na wapinzani wao. Hata hivyo, katika mechi ya hivi karibuni walipoteza mbele ya Athletic Club kwa mabao 2-0, jambo linaloonyesha kuwa bado wana kazi ya kufanya hasa wanapokutana na timu kali.
Celta wanategemea sana mashambulizi ya haraka na mpangilio mzuri wa uwanja wa kati ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wenye historia ndefu kama Real Sociedad.
Mechi kati ya timu hizi mbili zimekuwa na ushindani mkubwa. Katika michezo 33 iliyopita, Real Sociedad wameshinda mara 17, Celta wameshinda mara 7, na mechi 9 zimeishia sare. Takwimu hizi zinaonyesha ubora wa Real Sociedad wanapocheza nyumbani, ingawa Celta wana uwezo wa kuvuruga mipango ya wenyeji kwa mashambulizi ya kasi, hasa kupitia pembeni mwa uwanja.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kwa upande wa majeruhi, Real Sociedad watakosa huduma za beki wao Álvaro Odriozola kutokana na jeraha, jambo linaloweza kuathiri mpangilio wao wa ulinzi. Celta Vigo kwa sasa hawana taarifa za majeruhi wa maana, hali inayowapa nafasi nzuri ya kuweka kikosi chao bora zaidi uwanjani.
Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Real Sociedad wanacheza nyumbani na wana historia nzuri dhidi ya Celta, lakini hali yao ya sasa ya ligi inawapa shinikizo la kutafuta ushindi wa lazima. Celta Vigo, kwa upande wao, watakuja na lengo la kutumia udhaifu wa ulinzi wa wenyeji ili kuchukua angalau pointi moja au tatu kutoka Reale Arena.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...