Red Cross Mkoa wa Simiyu imeendesha mafunzo maalum ya huduma ya kwanza kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 08 Septemba 2026 chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Red Cross Mkoa wa Simiyu, Sitta Tumma.

Lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma wa kujitolea na askari wa zimamoto ili wawe tayari kutoa msaada wa haraka wakati wowote na mahala popote. Hii ni maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua kubwa za El-Nino zinazotabiriwa kuanza Oktoba 2026.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Red Cross Mkoa wa Simiyu ilisema imechukua jukumu la kuhakikisha jamii inakuwa tayari kukabiliana na majanga. Taasisi hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha utamaduni wa kujitolea kwa kuzingatia Kanuni Saba za Kimataifa za Red Cross ambazo ni Ubinadamu, Uadilifu, Kutokupendelea, Uhuru, Kujitolea, Umoja na Ulimwengu.

Katika mafunzo hayo ya pamoja, washiriki walipata elimu ya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, kuzuia damu, kutoa huduma kwa waliopata majeraha madogo na makubwa, pamoja na namna ya kuwasili katika tukio haraka na kwa usalama.

Watoa mafunzo walikuwa ni Hamis Shaban Mrisho, Barnabas Charles Daud, Aziz Abeod na Isaya Mganule. Walitoa masomo mbalimbali kwa vitendo na kinadharia ili kuhakikisha kila mshiriki anaelewa na anaweza kutekeleza.

Mafunzo haya yanakuja wakati Serikali ikitangaza kuwa mvua za El-Nino zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba na kuleta athari katika baadhi ya mikoa ikiwemo Simiyu. Hivyo ushirikiano kati ya Red Cross na Jeshi la Zimamoto unalenga kuhakikisha hakuna upotevu wa maisha utakaotokea wakati wa majanga hayo.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...