Na Victor Masangu, Bagamoyo
MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo, Mhe. CPA Subira Khamisi Mgalu, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bagamoyo kwa ubunifu na mipango madhubuti inayolenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Mhe. Mgalu aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika Ofisi za TRA Bagamoyo, ambapo alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa TRA Bagamoyo, Mariam Omari.
Katika mazungumzo hayo, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu ongezeko la mapato, ukusanyaji wa kodi, mikakati ya kuvuka malengo ya ukusanyaji pamoja na umuhimu wa kuendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ulipaji wa kodi.
Mhe. Mgalu ameipongeza TRA Bagamoyo kwa kazi inayofanyika katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unaendelea kuimarika, akisema hatua hizo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya Taifa na Jimbo la Bagamoyo.
Aidha, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TRA na kuhamasisha wananchi kupitia mikutano yake mbalimbali kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati ili kuwezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mbunge huyo pia amempongeza Meneja wa TRA Bagamoyo, Mariam Omari, kwa moyo wa kujitolea na kushirikiana na jamii, hususan katika kuchangia uboreshaji wa miundombinu katika Shule ya Msingi Ukuni.
Amesema ushiriki wa taasisi na watendaji katika shughuli za kijamii ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi na wananchi, hivyo unapaswa kuungwa mkono na kuendelezwa.
Mhe. Mgalu ameahidi kuwa balozi wa kuhamasisha ushirikiano kati ya wananchi, taasisi na wadau mbalimbali katika kuhakikisha juhudi za maendeleo ya Bagamoyo zinaendelea kuimarika.
Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi, taasisi na wananchi ni muhimu katika kuongeza uelewa kuhusu ulipaji wa kodi, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuchochea kasi ya maendeleo.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...