Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema haitambui matamko yanayohusu jezi mpya za timu za taifa, ikieleza kuwa mchakato wa kubadilisha jezi hizo haukuishirikisha Wizara licha ya maelekezo yaliyotolewa mwezi Februari 2026.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara hiyo leo September 18, 2026 imesema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, ameeleza kuwa Serikali inawekeza fedha nyingi katika maandalizi ya timu za taifa zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kwa kuzingatia Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, kuna umuhimu wa kuboresha jezi za timu za taifa ili ziakisi manufaa mapana kwa nchi.

Aidha, Wizara imesema Waziri Makonda ataandaa Kamati ya kuchunguza mkataba wa mzabuni wa jezi za timu za taifa, kwa lengo la kubaini manufaa yanayotokana na mkataba huo kwa timu hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo inazingatia ukweli kwamba Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuendesha timu za taifa, huku kukiwa na fursa ya mauzo ya jezi ambazo zinaweza kuchangia katika uendeshaji wa timu hizo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...