Na. Philipo Hassan - Mikumi
Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kikoboga uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi umefikia asilimia 75, ukihusisha jengo lenye uwezo wa kuhudumia abiria 160 kwa ujumla wanaowasili na wanaoondoka, njia ya kurushia na kutua ndege (Runway) yenye urefu wa kilomita 1.8, jengo la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, sehemu ya maegesho ya ndege na magari pamoja na kioski.

Kukamilika kwa uwanja huo kunatarajiwa kuongeza idadi ya watalii, kukuza mapato kwa Taifa na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa jamii inayozunguka hifadhi.
Akikagua mradi huo jana Septemba 17, 2026, Kamishna wa Uhifadhi, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Massana Mwishawa amemwelekeza mkandarasi “China Henan International Cooperation, Group Co. LTD (CHICO)” kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa ili kuleta tija kwa Taifa na jamii. Aidha, ameitaka Menejimenti ya Hifadhi kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi sambamba na kuimarisha utekelezaji wa shughuli za uhifadhi na utalii.
Pia, Kamishna Mwishawa alifanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara inayotokea lango la Kikoboga hadi lango la Chamgore yenye urefu wa kilometa 38, ambayo ukarabati wake umefikia asilimia 80. Ujenzi wa barabara hiyo unatekelezwa chini ya ufadhili wa fedha za Mfuko wa Kukuza Utalii nchini (TDL) unaosimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na kutekelezwa na TANAPA.
Barabara hiyo itaunganisha Lango la Chamgore lililopo upande wa Kilosa linalotarajiwa kuanza kujengwa mwaka huu, hivyo itaongeza wigo mkubwa wa mtandao wa njia za utalii ndani ya hifadhi kwa kuwawezesha watalii watakokuwa wanashuka na treni ya mwendo kazi (SGR) mjini Kilosa na kuingia hifadhini.
Hifadhi ya Taifa Mikumi ni miongoni mwa hifadhi zinazovutia katika ukanda wa mashariki mwa Tanzania, ikifahamika kwa urahisi wa kufikika na fursa ya kuona wanyamapori kwa haraka. Miongoni mwa vivutio vyake ni pamoja na makundi ya tembo, nyati, simba na twiga, pamoja na mandhari ya kuvutia na fursa nzuri ya kufanya utalii wa ndege.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...