Farida Mangube Morogoro
Zaidi ya vijana 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamepewa mafunzo ya kuzalisha vifaranga bora vya samaki, ikiwa ni fursa ya kuwawezesha kuongeza kipato kupitia ufugaji na kujenga ujuzi katika sekta ya ufugaji wa samaki.
Mafunzo hayo ya siku nne yanatolewa kwa vijana na wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji wa samaki, kwa lengo la kuwapa ujuzi wa kuzalisha vifaranga bora na hatimaye kuvisambaza kwa wafugaji wengine.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Janeth Rukanda, amesema Serikali imeamua kuwawezesha vijana kwa kuwa ongezeko la shughuli za ufugaji wa samaki limeongeza mahitaji ya vifaranga bora nchini.
Amesema mafunzo hayo yatawasaidia vijana kufanya ufugaji kwa tija, kuongeza kipato na kuwa wazalishaji wa vifaranga watakaoweza kuwahudumia wafugaji wengine katika maeneo mbalimbali.
“Lengo la Serikali ni kuwajengea uwezo vijana wengi zaidi juu ya uzalishaji wa vifaranga bora,” amesema Rukanda.
Kwa mujibu wa Rukanda, tafiti za mwaka 2020 hadi 2025 zinaonyesha kuwa uzalishaji wa vifaranga umeongezeka, lakini ongezeko la mahitaji limeendelea kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya ufugaji wa samaki.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Samaki (FETA), Makao Makuu, Mezia Mparazo, amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo wanayopewa ili waweze kutumia ujuzi huo katika shughuli zao za uzalishaji.
“Msipokuwa makini na kuwasikiliza ipasavyo wakufunzi, mtaondoka bila kupata maarifa ya kutosha. Hili litakuwa hasara kwenu na kwa Serikali, kwa sababu mafunzo kama haya yanatumia gharama kubwa,” alisema Mparazo.
Kwa upande wao, Gojo Muhammed na Radhia Suleiman, ambao ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo, wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata ujuzi wa uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki.
Wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza ujuzi, kuboresha shughuli zao za ufugaji na kutengeneza fursa zaidi za kiuchumi kupitia uzalishaji wa vifaranga vya samaki.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...